Hadithi za Maandiko
Kuhusu Mafundisho na Maagano


“Kuhusu Mafundisho na Maagano,” Simulizi Kutoka Mafundisho na Maagano (2024)

“Kuhusu Mafundisho na Maagano,” Simulizi Kutoka Mafundisho na Maagano

Utangulizi

Kuhusu Mafundisho na Maagano

Bwana anazungumza tena

Yesu Kristo akiwatokea watu katika Amerika ya kale.

Baba Yetu wa Mbinguni anatupenda. Anataka tufanye maagano, au ahadi, pamoja Naye ili Aweze kutubariki. Alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, kuwa Mwokozi wetu na kutusaidia kurudi Kwake.

Nabii wa kale akiandika kwenye hati ya kukunja.

Mungu pia hutuma manabii kutufundisha kuhusu Yesu Kristo na amri Zake. Manabii humtumikia Yesu Kristo na kusaidia kuongoza Kanisa Lake.

Musa akiwa ameshikilia Amri Kumi.

Yesu huwaambia manabii nini cha kutufundisha. Maneno ya manabii kutoka zamani za kale yameandikwa katika maandiko kama Biblia na Kitabu cha Mormoni.

Joseph Smith akijiuliza ni desturi ipi ya kidini ya kuifuata.

Kwa miaka mingi baada ya Yesu kuwepo duniani, hakukuwa na manabii. Watu hawakuwa wakifanya na kushika maagano na Mungu. Kanisa la Yesu Kristo halikuwepo duniani.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanamtokea Joseph Smith.

Lakini Mungu alimwita Joseph Smith kuwa nabii. Joseph alikuwa kijana mdogo tu, lakini Mungu alikuwa na kitu muhimu sana kwake kufanya.

Watu wakinyanyua mikono yao kuwakubali Joseph na Oliver kama viongozi wa Kanisa.

Joseph Smith alifundisha kuhusu Yesu. Alisaidia kuanzisha Kanisa la Yesu. Yesu alimfundisha Joseph Smith injili Yake na jinsi ya kuongoza Kanisa Lake.

Familia ikisoma Mafundisho na Maagano.

Mambo mengi Yesu aliyowaambia Joseph Smith yameandikwa katika Mafundisho na Maagano. Mafundisho na Maagano ni kitabu cha maandiko kama Biblia na Kitabu cha Mormoni.

Kielelezo cha upimaji kikionyesha jinsi watu walivyoshawishiwa na Mafundisho na Maagano.

Simulizi Kutoka Mafundisho na Maagano zinaelezea jinsi Yesu alivyorudisha, au kurejesha, Kanisa Lake, kwa msaada kutoka kwa Nabii Joseph Smith na wengine. Waumini wa Kanisa wanaitwa Watakatifu. Masimulizi haya huonyesha kwamba Mungu anawapenda watoto Wake ulimwenguni kote. Anataka kutubariki tunapofanya maagano na Yeye.