Hadithi za Maandiko
Joseph na Hyrum Wanatoa Uhai Wao kwa ajili ya Injili


“Joseph na Hyrum Wanatoa Uhai Wao kwa ajili ya Injili,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Joseph na Hyrum Wanatoa Uhai Wao kwa ajili ya Injili,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Machi–Juni 1844

Joseph na Hyrum Wanatoa Uhai Wao kwa ajili ya Injili

Nabii anafariki, lakini kazi ya Bwana inaendelea

Joseph Smith anapitisha funguo za ukuhani kwa Mitume wa Kanisa.

Joseph Smith alikuwa na wasiwasi. Ni nini kingetokea kwa Kanisa kama yeye angekufa? Alitaka kuhakikisha kazi ya Bwana ingeendelea kusonga mbele. Hivyo aliwakusanya Mitume na kuwapa funguo za ukuhani ambazo Yesu Kristo alikuwa amempa. Hii ilimaanisha kwamba Mitume wangeweza kuongoza Kanisa la Bwana na kufanya kazi Yake. Hii ilimsaidia Joseph kuhisi vizuri zaidi.

Watakatifu, 1:519-20

Tukio katika Nauvoo likionyesha baadhi ya watu waliomkasirikia Joseph.

Lakini kulikuwa na watu wengi ambao walimkasirikia Joseph. Baadhi ya watu hata walitaka kumuua. Hawakupenda kile alichokuwa akifundisha. Waliandika kumhusu yeye katika gazeti ili kuwafanya watu kumkasirikia zaidi Joseph na Kanisa. Baadhi yao walitaka kuishambulia Nauvoo.

Watakatifu, 1:526–28, 530, 533

Joseph akiwa pamoja na familia yake

Joseph na viongozi wengine huko Nauvoo walikiharibu kiwanda cha uchapishaji ili kuzuia chuki kuenea. Hii iliwafanya watu wawe na hasira zaidi. Gavana alimwambia Joseph aende katika mji wa Carthage ili jaji aweze kuamua kama alikuwa amevunja sheria. Joseph alijua kama angeenda Carthage, watu wangemuua.

Mafundisho na Maagano 135:4; Watakatifu, 1:533–37, 539–41

Joseph akisema kwaheri kwa familia yake na kuondoka kwenda Carthage.

Lakini Joseph pia alitaka Watakatifu wawe salama. Kama angeenda Carthage, labda watu wangewaacha Watakatifu huko Nauvoo peke yao. Joseph aliamua kwenda. Alimbariki Emma na watoto wake, akawabusu akiwaaga, na akaondoka kwenda Carthage.

Watakatifu, 1:542–44

Joseph na Hyrum wakiondoka kwenda Nauvoo.

Kaka yake Joseph alikwenda pamoja naye. Hivyo John Taylor, Willard Richards na marafiki wengine. Walipokuwa wakiondoka, Joseph alisimamisha farasi wake na kutazama nyuma huko Nauvoo. “Hapa ni mahali pa kupendeza zaidi na watu bora chini ya mbingu,” alisema.

Watakatifu, 1:543–45

Mandhari kutoka Gereza la Carthage: Hyrum akisoma Kitabu cha Mormoni na Joseph akiwahubiria walinzi.

Walipowasili Carthage, waliwekwa jela. Walipokuwa jela, Hyrum aliwasomea kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Joseph aliwaambia walinzi kwamba Kitabu cha Mormon ni cha kweli.

Watakatifu, 1:546

John Taylor akiimba wimbo wa dini.

Kuwafariji rafiki zake, John Taylor aliimba wimbo kuhusu Yesu. Ilikuwa ya kupendeza, na Hyrum alimuomba aimbe tena.

Watakatifu, 1:549

Genge la watu wenye fujo wakivunja na kuingia ndani ya jela.

Baadaye siku hiyo, wanaume wenye hasira wakiwa na bunduki walikimbia na kuingia jela. Waliusukuma mlango na kuanza kurusha risasi ndani ya chumba ambapo Joseph na rafiki zake walikuwepo. John Taylor aliumizwa vibaya. Hyrum na Joseph waliuawa.

Mafundisho na Maagano 135:1–2; Watakatifu, 1:550–52

Watakatifu wakiomboleza kifo cha Joseph na Hyrum.

Watakatifu walikuwa na huzuni sana walipogundua kwamba Joseph na Hyrum walikuwa wamekufa. Lakini walijua kwamba kumuua Nabii hakutazuia Kanisa. Ni Kanisa la Mwokozi, na Bwan angeendelea kuliongoza. Kanisa lingeendelea kukua na kubariki watoto wa Mungu ulimwenguni kote.

Watakatifu, 1:553–59