“Kanisa la Yesu Kristo Linaanzishwa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Kanisa la Yesu Kristo Linaanzishwa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Apili 1830
Kanisa la Yesu Kristo Linaanzishwa
Mkutano wa Kanisa wenye shangwe
Kitabu cha Mormoni sasa kilikuwa kimechapishwa, na nguvu ya ukuhani wa Mungu ilikuwa duniani tena. Bwana alimwambia Joseph Smith ilikuwa ni wakati wa kuanzisha Kanisa la Yesu Kristo.
Saints, 1:84
Mnamo Aprili 6, 1830, takribani wanawake na wanaume 40 walikuja nyumbani kwa familia ya Whitmer kuanzisha Kanisa. Bwana alikuwa amewaita Joseph na Oliver kuongoza Kanisa Lake. Joseph na Oliver waliwaomba watu wanyanyue mikono yao ili kuonyesha kwamba waliwakubali kama viongozi wao.
Mafundisho na Maagano 20:1–3; Saints, 1:84
Kisha, Joseph na Oliver walibariki sakramenti. Waliitoa kwa watu ili kuwasaidia kumkumbuka Yesu Kristo. Joseph na Oliver kisha waliweka mikono yao juu ya vichwa vya watu ambao walikuwa wamebatizwa. Waliwathibitisha kuwa waumini wa Kanisa na kuwapatia kipawa cha Roho Mtakatifu.
Mafundisho na Maagano 20:75–79; Saints, 1:85
Bwana alimpa Joseph ujumbe kwa ajili ya Kanisa jipya. Aliwaambia waandike kile kilichotokea Kanisani. Alisema kwamba Joseph Smith alikuwa Nabii Wake. Aliwaahidi waumini wa Kanisa kwamba kama watafuata amri alizompa Joseph, Yeye angewabariki. Ibilisi asingeweza kuwa na nguvu juu yao.
Mafundisho na Maagano 21:1–6; Saints, 1:85
Watu walikuwa na furaha sana kuwa na Kanisa la Yesu Kristo! Baada ya mkutano, watu wengi walibatizwa, wakiwemo mama na baba yake Joseph Smith. Wakati baba yake alipotoka majini, Joseph alimpa kumbatio kubwa. “Nimeishi kumwona baba yangu akibatizwa katika kanisa la kweli la Yesu Kristo!” alisema.
Saints, 1:86
Baadaye usiku huo, Joseph alikwenda msituni kuwa peke yake. Moyo wake ulijaa shangwe. Ilikuwa miaka 10 tangu alipomwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa mara ya kwanza. Mengi yalikuwa yametokea tangu wakati huo. Joseph alikuwa mwenye shukrani nyingi kwamba ameweza kusaidia kurejesha, au kurudisha tena, Kanisa la Yesu Kristo!
Saints, 1:86