“Muungano wa Usaidizi,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Muungano wa Usaidizi,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Machi 1842
Muungano wa Usaidizi
Wanawake wa Nauvoo wanamtumikia Bwana
Margaret Cook aliishi huko Nauvoo. Alifanya kazi kwa Sarah Kimball, akimsaidia kazi ya kushona. Alipokuwa akifanya kazi, walipenda kuzungumza kuhusu hekalu jipya linalojengwa huko Nauvoo. Walifurahi kwa ajili ya hekalu hilo.
Watakatifu, 1:447
Siku moja, Margaret aligundua kwamba wengi wa wanaume wanaojenga hekalu walikuwa na nguo ambazo zilikuwa za zamani na zilizochakaa. Alijiuliza kama yeye na Sara wangeweza kufanya kazi pamoja kushona mashati mapya kwa ajili ya wanaume hao. Sara alipenda wazo hilo. Yeye na Margaret walizungumza na wanawake wengine kuhusu kuunda kikundi ili kuwasaidia wafanyakazi hao.
Watakatifu, 1:447–48
Nabii Joseph alisema Bwana alifurahia wazo lao, na alikuwa na kitu kizuri zaidi kwao. Joseph aliwaalika wanawake kukutana naye mnamo Machi 17, 1842. Akitumia mamlaka ya ukuhani, aliwapanga wanawake wa Kanisa. Waliamua kukiita kikundi chao kama Muungano wa Usaidizi wa Wanawake wa Nauvoo.
Watakatifu, 1:448, 450–51
Joseph aliwaomba Muungano wa Usaidizi kuwasaidia watu kujiandaa kwa ajili ya baraka za hekalu na uzima wa milele. Wanapaswa kuwa mifano ya kumfuata Yesu.
Watakatifu, 1:451
Joseph pia alisema Muungano wa Usaidizi unapaswa kuwatafuta watu ambao walikuwa masikini na kuwasaidia. Hata wanawake waliokuwa maskini walitaka kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Watakatifu, 1:449
Muungano wa Usaidizi ulianzishwa. Emma Smith aliitwa kuwa rais. Aliwaita washauri wawili, Sarah Cleveland na Ann Whitney. Pia alimwita katibu, Eliza R. Snow.
Watakatifu, 1:450
Bwana alimsaidia Emma kutimiza wito wake. Emma aliwafundisha wanawake kwamba wangeweza kufanya mambo makubwa katika huduma ya Bwana. Alitaka kila mmoja wao kutafuta njia za kufanya mema. Muhimu zaidi, aliwaambia, ilikuwa ni kuwapenda watu wengine jinsi Yesu alivyofanya. Wanawake wengi katika Nauvoo walijiunga na Muungano wa Usaidizi.
Mafundisho na Maagano 25:3, 7; Watakatifu, 1:451
Waliwasaidia watu kujitayarisha kwa ajili ya baraka za hekaluni na kusaidia familia nyingi ambazo zilikuwa na uhitaji huko Nauvoo. Tangu hapo, wanawake ulimwenguni kote wamejiunga na Muungano wa Usaidizi. Wanaendelea kuwahudumia watu na kuwasaidia kupokea baraka za hekaluni.
Watakatifu, 1:451