Hadithi za Maandiko
Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo


“Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

1841–1843

Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo

Wakitembea kwa imani katika Bwana

Jane Manning akibatizwa.

Jane Manning na familia yake waliishi katika mahali ambapo baadhi ya watu hawakuwapenda na walitendea vibaya kwa sababu ya rangi ya ngozi zao. Siku moja, Jane alisikia mafundisho ya wamisionari. Alijua ujumbe wake ulikuwa wa kweli. Jumapili iliyofuata tu, yeye alibatizwa.

Saints, 1:500–501

Jane na familia yake wakianza safari yao kwenda Nauvoo.

Familia ya Jane pia ilijiunga na Kanisa. Bwana aliwataka Watakatifu kukusanyika pamoja Nauvoo. Jane alimpenda Bwana. Yeye na familia yake walitaka kuwa pamoja na Watakatifu wengine. Kwa hiyo walianza safari yao kwenda Nauvoo.

Mafundisho na Maagano 124:25; Saints, 1:501

Jane na familia yake wamekataliwa kusafiri kwenye mashua.

Kwa sehemu ya safari yao, walisafiri kwa mashua. Watu wengi kwenye mashua wangeweza kulipia usafiri mwishoni mwa safari. Lakini baadhi ya watu waliiambia familia ya Jane walipaswa kulipa mwanzoni. Hawakuwa na pesa ya kutosha. Wanaume waliwafanya watoke kwenye mashua, na iliondoka bila wao.

Saints, 1:501

Jane na familia yake wakitembea kwenda Nauvoo.

Familia ya Jane bado ililazimika kusafiri maili 800, au kilomita 1,300. Iliwabidi wavuke kijito chenye kina kirefu bila daraja. Iliwabidi kulala nje. Hali ya hewa mara nyingi ilikuwa baridi sana. Lakini familia ya Jane ilidhamiria kufika Nauvoo. Walijishangilia kwa kuimba walipokuwa wakitembea.

Saints, 1:501, 505–6

Jane akimuuguza mwanafamilia.

Jane na familia yake walitembea na kutembea mpaka viatu vyao vikachakaa na miguu yao ikaumia. Lakini walipomwomba Mungu kwa ajili ya msaada, Yeye aliiponya miguu yao.

Saints, 1:505

Jane na familia yake wakimsaidia mtoto mgonjwa.

Waliwasaidia watu waliokutana nao katika safari yao. Walisaidia hata kumponya mtoto mgonjwa kwa sababu ya imani yao.

Saints, 1:505–6

Emma na Joseph wanamkaribisha Jane nyumbani mwao.

Hatimaye, Jane na familia yake walifika Nauvoo! Walikuwa wamechoka na walihitaji mahali pa kukaa. Kwa hiyo walikwenda nyumbani kwa Emma na Joseph. Wakati Joseph aliposikia yote waliyokuwa wamepitia, alimwambia Jane, “Mungu akubariki. Nyinyi mko miongoni mwa marafiki sasa.” Joseph na Emma walimwalika Jane kuishi pamoja nao.

Saints, 1:506