Hadithi za Maandiko
Hawn’s Mill


“Hawn’s Mill,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Hawn’s Mill,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Oktoba 1838–Februari 1839

Hawn’s Mill

Shambulio na muujiza

Willard Smith na familia yake katika Hawn’s Mill.

Willard Smith alikuwa na umri wa miaka 11. Familia yake iliishi katika Hawn’s Mill, Missouri, pamoja na Watakatifu wengine. Punde Watakatifu walitaka kukusanyika pamoja na Watakatifu huko Far West.

Mafundisho na Maagano 115:7–8; Saints, 1:347–48

Watu wakija kuwashambulia Watakatifu huko Hawn’s Mill.

Siku moja, Willard alikuwa pamoja na baba yake na kaka zake, Sardius na Alma. Ghafla, walisikia milio ya risasi na mayowe. Watu walikuwa wamekuja kuwashambulia Watakatifu.

Saints, 1:348–49

Watakatifu wakijificha kutoka kwa washambuliaji katika Hawn’s Mill.

Kila mtu alikimbia kutafuta usalama. Wanaume na watoto wengi walijificha katika duka la mhunzi. Baba na kaka zake Willard waliingia ndani pia, lakini Willard alipoteleana nao. Alijificha nyuma ya rundo la kuni. Alisikia milio ya risasi kila mahali

Saints, 1:349, 353

Willard akikimbia.

Willard alikimbia kutoka mahali hadi mahali ili kujificha. Hatimaye milio ya risasi ilikoma. Washambuliaji walikuwa wameondoka kutoka Hawn’s Mill.

Saints, 1:353

Willard katika duka la mhunzi.

Willard alikuja kwenye duka la mhunzi ili kuitafuta familia yake. Baba yake na Sardius walikuwa wameuawa. Lakini Alma kaka mdogo wa Willard alikuwa bado hai.

Saints, 1:353

Willard akimbeba kaka yake mdogo Alma.

Alma alikuwa amepigwa risasi kwenye nyonga. Alikuwa ameumizwa vibaya sana. Willard alimchukua Alma na kumbeba hadi kwenye hema la familia yao.

Saints, 1:353–54

Amanda Smith akisali kwa ajili ya mwanawe Alma.

Mama yake Willard, Amanda, hakujua jinsi ya kusaidia nyonga ya Alma. Lakini alijua Mungu alijua. Alisali, na akasikia sauti inamwambia nini cha kufanya.

Saints, 1:354

Amanda akikitibu kidonda cha Alma.

Amanda aliosha kidonda cha Alma kwa majivu. Kisha akaponda mzizi fulani wa mti na kuuweka kwenye jeraha lake. Alifunga nyonga yake kwa kitambaa. “Lala hivyo, na usiondoke,” alisema, “na Bwana atakufanyia nyonga nyingine.”

Saints, 1:354–55

Amanda akisali kwa ajili ya msaada.

Baadaye, gavana wa Missouri alisema kwamba Watakatifu ilibidi waondoke jimboni au wangeuawa. Lakini nyonga ya Alma bado haijatapata nafuu. Amanda alisali na kumwomba Bwana msaada. Sauti ilimwambia kwamba Yesu kamwe asingeiacha familia yake. Amanda alihisi kama hakuna ambacho kingeweza kumuumiza.

Mafundisho na Maagano 88:83; Saints, 1:372, 378–79

Alma akitembea baada ya nyonga yake kuponywa.

Punde baada ya kusali, Amanda aliwasikia watoto wake wakipiga mayowe. Alikimbia kuwatafuta, na alipofanya hivyo, Alma alikuwa akikimbia. “Mimi ni mzima, Ma, mimi ni mzima!” alisema. Nyonga yake ilikuwa imeponywa! Ulikuwa ni muujiza kutoka kwa Bwana. Amanda na watoto wake waliondoka Missouri kutafuta mahali salama pamoja na Watakatifu wengine.

Saints, 1:379