Hadithi za Maandiko
Mitume Wanahudumu Misheni huko Uingereza


“Mitume Wanahudumu Misheni huko Uingereza,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Mitume Wanahudumu Misheni huko Uingereza,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Julai 1838–Julai 1841

Mitume Wanahudumu Misheni huko Uingereza

Kutumaini katika ahadi za Bwana

Joseph Smith akipokea ufunuo wa kuwaita Mitume wa Kanisa kwenda kwenye misheni huko Uingereza.

Katika ufunuo kwa Joseph Smith, Bwana aliwaita Mitume kwenda kwenye misheni kuvuka bahari hadi Uingereza. Ingawa ilikuwa vigumu kwa Joseph kuwa na Mitume mbali sana, alimtumaini Bwana. Ilikuwa vigumu pia kwa Mitume kuacha familia zao. Lakini Bwana aliahidi kuwabariki.

Mafundisho na Maagano 118

Heber Kimball na familia yake.

Heber C. Kimball na mkewe, Vilate, walikuwa na familia changa. Walikuwa na mtoto mchanga ambaye alikuwa na umri wa mwezi mmoja tu. Washiriki wengi wa familia yao walikuwa wagonjwa sana.

Watakatifu, 1:405

Brigham Young akijiandaa kuondoka kwenda kwenye misheni yake.

Brigham Young pia alikuwa mgonjwa, na familia yake ilikuwa masikini. Lakini mke wa Brigham, Mary Ann, alimwambia, “Nenda ukatimize misheni yako, na Bwana atakubariki.”

Watakatifu, 1:404–5

Brigham Young anakaa na Heber C. Kimball.

Brigham alianza kwenda, lakini wakati alipofika nyumbani kwa Heber, alikuwa dhaifu sana hakuweza kutembea. Alikaa na familia ya Heber kwa siku chache.

Watakatifu, 1:405

Mary Ann Young akiwatunza Brigham na Heber.

Mary Ann alikuja kumtunza Brigham hadi yeye na Heber walipopona vya kutosha kuondoka. Wote walikuwa wadhaifu sana, lakini walitaka kuhubiri injili.

Watakatifu, 1:405

Brigham na Heber wakiondoka kwenda kwenye misheni yao.

Heber na Brigham walisema kwaheri kwa wake zao na kupanda nyuma ya mkokoteni. Walihisi vibaya kuziacha familia zao wakiwa wagonjwa na masikini. Wakati mkokoteni ulipokuwa ukiondoka, Heber alimwambia Brigham, “Hii ni ngumu sana.” Alitaka kuzisaidia familia zao kuhisi ujasiri. Heber alimwomba dereva wa mkokoteni kusimama.

Watakatifu, 1:405–6

Brigham na Heber wakisimama ili kusema kwaheri.

Kutoka ndani ya nyumba, Vilate alisikia kelele. Alikuja mlangoni, ambapo Mary Ann alikuwa amesimama. Waliwaona Heber na Brigham wakiwa wamesimama nyuma ya mkokoteni, wakipunga kofia zao hewani na wakipiga kelele, “Huree! Huree! Huree kwa Israeli!” Wanawake walijibu: Kwaherini! Mungu awabariki!”

Watakatifu, 1:406

Brigham na Heber wakihubiri huko Uingereza.

Baada ya safari ndefu ya kuvuka bahari, Heber na Brigham waliwasili huko Uingereza. Pamoja na Mitume wengine, waliwafundisha watu wengi kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Watu wengi walibatizwa na kujiunga na Kanisa la Mwokozi.

Watakatifu, 1:408–11

Watakatifu wakisafiri ili kuishi huko Nauvoo.

Wengi wa watu waliobatizwa huko Uingereza walihamia Nauvoo ili kusaidia kujenga jiji na hekalu. Bwana alitimiza ahadi Yake ya kuzitunza familia za Heber na Brigham wakati walipokuwa wakimtumikia Yeye kama wamisionari.

Watakatifu, 1:437–39