Hadithi za Maandiko
Ndoa ya Mitala


“Ndoa ya Mitala,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Ndoa ya Mitala,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

1831–1890

Ndoa ya Mitala

Amri kwa muda

Joseph Smith akijifunza maandiko na kufikiria kuhusu ndoa ya mitala.

Wakati Nabii Joseph alipokuwa akijifunza Biblia, alisoma kuhusu manabii kama Ibrahimu na Musa ambao walikuwa wameoa na zaidi ya mke mmoja. Joseph alikuwa na maswali mengi. Hivyo aliamua kusali na kumuuliza Bwana.

Mafundisho na Maagano 132:1; Saints, 1:121, 503

Joseph anajifunza kwamba watu wanapaswa kuwa katika ndoa ya mitala ikiwa tu wameamriwa na Mungu.

Bwana alisema kwamba kwa kawaida mwanaume alipaswa kuwa na mke mmoja tu. Lakini wakati mwingine Bwana alimwamuru mtu kuoa mke zaidi ya mmoja. Hii iliitwa ndoa ya mitala. Bwana alimwambia Joseph kwamba watu Wake wanapaswa kuwa tu katika ndoa za mitala kama Yeye ataamuru.

Yakobo 2:27–30; Mafundisho na Maagano 132:34–39; Saints, 1:121, 290–91, 489–90, 503

Joseph akisali kuhusu amri hii.

Miaka kadhaa baadaye, Bwana alimwambia Joseph na baadhi ya Watakatifu wengine kuwa katika ndoa za mitala. Haikuwa rahisi kuishi amri hii.

Saints, 1:290–91, 444–46

Muumini wa Kanisa anasimama mbele ya hakimu kwa sababu yuko katika ndoa ya mitala.

Serikali ilitoa sheria dhidi ya ndoa za mitala. Baadhi ya Watakatifu, ikijumuisha viongozi wa Kanisa, waliwekwa gerezani.

Saints, 2:501–4

Waumini wa Kanisa wanakubali amri kwamba wasifanye tena ndoa ya mitala.

Mnamo 1890, Bwana alimwambia Wilford Woodruff, Rais wa Kanisa, kwamba wanaume wasioe tena zaidi ya mke mmoja. Viongozi wa Kanisa walishiriki amri hii na Watakatifu. Hii bado ni amri ya Bwana leo—mwanaume lazima aoane na mke mmoja tu.

Tamko Rasmi 1; Saints, 2:598–601, 607–9