Hadithi za Maandiko
Familia ya Jackson


“Familia ya Jackson,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Familia ya Jackson,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Mei–Novemba 1856

Familia ya Jackson

Safari ya imani na uokozi

Familia ya Jackson ikiabiri meli huko Liverpool, Uingereza.

Baada ya kundi la kwanza la Watakatifu kwenda Bonde la Salt Lake, maelfu ya Watakatifu wengine walikwenda pia. Walisafiri kwa muda mrefu, na Bwana aliwasaidia. Familia moja iliyofanya safari hiyo ilikuwa familia ya Jackson. Waliondoka nyumbani kwao Uingereza na walifurahia kwenda kuwasaidia Watakatifu kujenga Sayuni.

Mafundisho na Maagano 136:1–11; Saints, 2:222–23

Akina Jackson wakisafiri kwa meli.

Akina Jackson walivuka bahari kwenye meli. Kisha wakaabiri gari moshi kwenda Bonde la Salt Lake. Wangelazimika kutembea umbali wote uliyobakia.

Saints, 2:222–23

Akina Jackson wakipakia mkokoteni wao.

Walitengeneza mkokoteni mdogo wa kubeba chakula chao, nguo, na vitu vingine walivyotaka kuvileta. Watakatifu wengi walifika salama kwenye bonde kwa njia hii.

Saints, 2:223–26

Akina Jackson wakisafiri magharibi kwa mkokoteni wao.

Elizabeth na Aaron Jackson walivuta mkokoteni wao mzito. Watoto wao, Martha, Mariamu, na Aaron Mdogo, walitembea. Ilikuwa kazi ngumu. Walitumaini kufika bonde kabla ya majira ya baridi. Lakini wakati wa majira ya majani kupuputika yalipofika, bado walikuwa na safari ndefu ya kwenda. Ilikuwa inaanza kuwa baridi, na walikuwa wakiishiwa na chakula.

Saints, 2:223–26, 229, 231–32

Brigham Young anawaomba Watakatifu huko Salt Lake kuwasaidia Watakatifu waliokuwa wakisafiri kuja magharibi.

Katika Jiji la Salt Lake, Brigham Young waligundua kuhusu Watakatifu waliokuwa wanakisafiri kuja bondeni. Alikuwa na wasiwasi juu yao. Siku iliyofuata kanisani, alimwambia kila mtu kwamba Watakatifu hawa walikuwa katika matatizo. Aliwaomba wajaze mikokoteni kwa vitu ambavyo Watakatifu wangehitaji. “Nendeni mkawalete wale watu,” alisema.

Saints, 2:229–30

Watakatifu katika Salt Lake wakikusanya vitu ili kuwasaidia Watakatifu waliokuwa wakisafiri kuja magharibi.

Wanawake katika mkutano walivua soksi zao za joto na kuziweka kwenye magari ya kukokotwa na maksai. Wengine walitoa chakula chao, mablanketi, viatu, na nguo. Siku mbili baadaye, zaidi ya wanaume 50 na magari 20 ya kukokotwa na maksai yaliondoka bondeni ili kwenda kusaidia.

Saints, 2:230

Aaron Jackson na Watakatifu wengine wakivuka Mto North Platte.

Familia ya Jackson ilipoendelea kutembea, theluji ikaanza kuanguka. Aaron akawa mgonjwa sana. Ilikuwa vigumu kwake kutembea. Watakatifu walihitaji kuvuka mto ulioganda, na hii ilimfanya Aaron hata kuwa dhaifu zaidi. Usiku ule, Aaron alifariki. Kwa huzuni, familia yake ingepaswa kuendelea bila yeye.

Saints, 2:232–34

Jackson na Watakatifu wengine wakivuta mikokoteni yao kwenye theluji.

Asubuhi iliyofuata, theluji zaidi ilikuwa ardhini. Jackson na Watakatifu wengine walisukuma na kuvuta mikokoteni yao kupitia theluji. Walisali kila siku kwamba Mungu angesaidie.

Mafundisho na Maagano 136:29; Saints, 2:234–35

Elizabeth Jackson akiota ndoto kuhusu mumewe.

Usiku mmoja, Elizabeth alikuwa na wasiwasi kuhusu watoto wake. Walikuwa na njaa, na wenye kuona baridi. Je, wangeliweza kufika bonde la Salt Lake? Alilala na kuota kwamba alimwona Aaron. Alisema, “Furahini, Elizabeth.” Alimwambia kwamba msaada ulikuwa unakuja.

Saints, 2:235–36

Watu wanawasili kuwasaidia Watakatifu.

Aaron alikuwa sahihi. Punde, wanaume kutoka Salt Lake waliwasili na magari yao ya kukokotwa na maksai. Waliwapa Watakatifu chakula na nguo. Watakatifu walishangilia na kucheka na kuwakumbatia wanaume hawa. Waliimba wimbo na kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa kujibu sala zao.

Mafundisho na Maagano 136:28; Saints, 2:236

Watakatifu wasafiri hatimaye wanawasili katika Bonde la Salt Lake.

Hatimaye walipofika kwenye bonde, ilikuwa Jumapili. Brigham Young aliwaambia waumini wa Kanisa katika Jiji la Salt Lake kwamba badala ya kwenda kanisani, wanapaswa kwenda kuwakaribisha Watakatifu ambao walikuwa wamewasili. Waliwasalimu Watakatifu wenye baridi na waliochoka na kuwaalika kukaa majumbani mwao.

Saints, 2:239–40