Hadithi za Maandiko
Joseph na Sidney Wanashambuliwa


“Joseph na Sidney Wanashambuliwa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Joseph na Sidney Wanashambuliwa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Februari 1832

Joseph na Sydney Wanashambuliwa

Watu wenye hasira wanajaribu kusimamisha kazi ya nabii wa Mungu

Watu wenye hasira wakizungumza karibu na moto unaowaka

Baadhi ya watu walipenda kile Joseph Smith alichokuwa anafundisha kuhusu Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na mbingu. Lakini watu wengine hawakupenda kile alichofundisha. Wachache wao walimkasirikia na walitaka kumzuia Joseph asifundishe.

Mafundisho na Maagano 76; Saints, 1:149–50

Emma na Joseph Smith wakimtunza mtoto wao mgonjwa.

Usiku mmoja, Joseph alikuwa amechelewa kulala akimsaidia Emma kumtunza mmoja wa watoto wao mapacha walioasiliwa. Mtoto yule alikuwa mgonjwa sana.

Saints, 1:150

Emma akiwabembeleza watoto wakati Joseph akilala.

Emma alimchukua yule mtoto na kumwambia Joseph apumzike. Alikuwa ahubiri asubuhi. Hatimaye, wote Joseph na Emma wakalala.

Saints, 1:150

Wanaume wakimburuza Joseph nje ya nyumba.

Ghafla, mlango ulifunguka, na kundi la wanaume wenye hasira wakaingia chumbani. Emma alipiga mayowe wakati wanaume hao walipomshika Joseph kwa mikono, miguu, na nywele. Walimburuza na kumtoa nje ya nyumba.

Saints, 1:150–51

Wanaume wakimnyakua Joseph wakati Sidney Rigdon akilala chini. ardhini

Joseph alijaribu kuponyoka kutoka kwa watu hao, lakini walimshika kwa nguvu. Joseph aliona kwamba wanaume hao pia walikuwa wamemvuta rafiki yake Sidney Rigdon kutoka nyumbani kwake.

Saints, 1:151

Wanaume wakimfunika Joseph kwa lami na manyoya.

Wanaume walichana nguo za Joseph na kumwagia lami ya moto, juu ya ngozi yake na nywele zake. Basi wakamfunika kwa manyoya na wakakimbia.

Saints, 1:152

Emma na rafiki zake wakiwatunza Joseph na Sidney.

Baada ya wale wanaume kuondoka, Joseph alijikokota kurudi nyumbani. Emma aliogopa alipomwona Joseph. Marafiki walioishi jirani walisikia kile kilichotokea na kuharakisha kuja kusaidia. Emma aliifuta lami kutoka kwenye ngozi ya Joseph. Kwa usiku ulio salia, Emma na marafiki zake walisaidia kuwatunza Joseph na Sidney

Mafundisho na Maagano 25:5; Saints, 1:153

Joseph akilihubiria kundi la Watakatifu

Siku iliyofuata, Joseph alikuwa bado katika maumivu mengi. Lakini alivaa nguo na kufundisha kundi la watu kuhusu Yesu Kristo. Baadhi ya wanaume waliomshambulia walimsikiliza akifundisha. Baadaye siku hiyo, Joseph aliwabatiza watu watatu. Aliendelea kufanya kazi ya Bwana, hata wakati watu walipojaribu kumzuia.

Mafundisho na Maagano 24:8; Saints, 1:153