“Neno la Hekima,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Neno la Hekima,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Februari 1833
Neno la Hekima
Sheria ya Bwana ya afya
Joseph Smith aliwaalika wanaume wachache katika Kanisa kuwa na mikutano pamoja naye kwenye ghorofa ya juu ya duka la Newel na Ann Whitney. Hapo walijifunza injili na masomo mengine, na walisali kama kikundi. Waliita mikutano hii Shule ya Manabii.
Mafundisho na Maagano 88:117–137; Saints, 1:166
Wengi wa wanaume hawa walivuta viko na kutafuna tumbaku wakati wa masomo. Moshi ulifanya hewa ya mawingu, na tumbaku ilifanya uchafu sakafuni. Baada ya mikutano, Emma Smith alipanda ghorofani kusafisha chumba. Kulikuwa kuchafu sana!
Saints, 1:167
Emma alisugua na kusugua sakafu, lakini madoa ya tumbaku hayakutoka. Aliongea na Joseph kuhusu uchafu huo.
Saints, 1:167
Joseph alimsikiliza Emma. Kumsikiliza kulimfanya ajiulize jinsi Bwana anavyojisikia kuhusu tumbaku.
Saints, 1:167
Hivyo Joseph alimwuliza Bwana kuhusu tumbaku. Bwana alimwambia Joseph kwamba alikuwa na Neno la Hekima kwa ajili ya Watakatifu.
Mafundisho na Maagano 89:1–9; Saints, 1:167
Bwana alisema Watakatifu hawapaswi kuvuta sigara, kutumia tumbaku, au kunywa pombe au “vinywaji vya moto,” ambavyo humaanisha kahawa na chai.
Mafundisho na Maagano 89:1–9; Saints, 1:167
Bwana pia aliwafundisha Watakatifu kwamba nafaka na matunda ni mazuri kwa kula. Pia alisema wangeweza wakati mwingine kula nyama.
Mafundisho na Maagano 89:10–17; Saints, 1:168
Bwana alimwambia Joseph kwamba Watakatifu waliochagua kutii Neno la Hekima Lake wangelindwa. Bwana aliahidi kuwabariki kwa afya, maarifa, na nguvu. Joseph aliwaambia wanaume katika Shule ya Manabii kuhusu Neno la la Hekima la Bwana.
Mafundisho na Maagano 89:18–21; Saints, 1:168
Wale wanaume chumbani walitupa tumbaku yao na viko vyao kwenye moto kuonyesha kwamba walitaka kutii Neno la Hekima la Bwana.
Saints, 1:168