“Watakatifu Wanajifunza kuhusu Ubatizo kwa niaba ya Wafu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Watakatifu Wanajifunza kuhusu Ubatizo kwa niaba ya Wafu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Agosti–Oktoba 1840
Watakatifu Wanajifunza kuhusu Ubatizo kwa niaba ya Wafu
Tumaini kwa ajili ya wanafamilia ambao hawakubatizwa
Jane Neyman aliishi Nauvoo. Alienda kwenye mazishi ambapo Joseph Smith alikuwa akizungumza. Mazishi hayo yalimfanya Jane afikirie kuhusu mwanawe Cyrus. Alikuwa amefariki na hakubatizwa. Jane alikuwa na wasiwasi kuhusu Cyrus. Alijua kwamba tunapaswa kubatizwa ili kuishi na Baba wa Mbinguni.
Watakatifu, 1:421
Joseph alijua jinsi Jane alivyohisi. Alikuwa anajiuliza jambo hilo hilo kuhusu kaka yake Alvin, ambaye pia alikuwa amefariki bila kubatizwa.
Watakatifu, 1:421
Katika mazishi hayo, Joseph alishiriki kitu ambacho Mungu alikuwa amemfundisha. Alisema kwamba wakati mtu fulani amefariki bila kubatizwa, tunaweza kubatizwa kwa niaba yao.
Watakatifu, 1:421
Jane alikuwa na furaha sana kusikia hili! Punde baada ya mazishi, alikwenda mtoni na mzee wa Kanisa. Alimbatiza kwa ajili ya Cyrus.
Watakatifu, 1:421
Wiki chache baadaye, Joseph aliwafundisha Watakatifu zaidi kuhusu ubatizo kwa niaba ya wafu. Alisema kwamba watu wengi waliokufa walitaka kubatizwa. Walitaka kumfuata Yesu. Walikuwa wakisubiri na kutumaini wanafamilia wao ambao bado walikuwa hai wabatizwe kwa niaba yao.
Mafundisho na Maagano 128:15-19; Watakatifu, 1:423
Watakatifu walikimbilia mtoni mara moja. Walibatizwa kwa ajili ya watu waliowapenda. Hyrum Smith alibatizwa kwa niaba ya Alvin. Baadaye, Bwana alifundisha kwamba ubatizo kwa niaba ya wafu unapaswa kufanyika hekaluni, mtu anapaswa kuweka kumbukumbu ya kila ubatizo, na wanaume wanapaswa kubatizwa kwa ajili ya wanaume na wanawake kwa ajili ya wanawake.
Mafundisho na Maagano 124:29- 32; 127:5–12; 128:1–9; Watakatifu, 1:424