Hadithi za Maandiko
Hiram Page na Ufunuo


“Hiram Page na Ufunuo,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Hiram Page na Ufunuo,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Septemba 1830

Hiram Page na Ufunuo

Watakatifu wanajifunza jinsi Mungu anavyoliongoza Kanisa Lake

Hiram Page akishiriki ujumbe wake na waumini wa Kanisa.

Hiram Page alikuwa rafiki wa Joseph Smith na Oliver Cowdery. Pia alikuwa mmoja wa mashahidi wanane wa mabamba ya dhahabu. Hiram alikuwa na jiwe, na aliamini kwamba Mungu alikuwa analitumia kumpa ujumbe, au ufunuo, kwa ajili ya Kanisa. Oliver na Watakatifu wengine waliamini mafunuo ya Hiramu yalitoka kwa Mungu.

Mafundisho na Maagano 28, kichwa cha habari cha sehemu; Saints, 1:97

Joseph Smith na wengine wakisikiliza mafundisho ya Hiram.

Mafunuo ya Hiram yalionekana kama maandiko. Lakini yalikuwa tofauti na kile Biblia inachofundisha. Pia yalikuwa tofauti na kile Bwana alichomwambia Nabii Joseph. Joseph hakuwa na uhakika wa nini cha kufanya.

Saints, 1:97

Joseph aliomba kwa ajili ya mwongozo.

Joseph alikaa usiku kucha akimwomba Mungu kwa ajili ya msaada. Alikuwa na hofu kuhusu kufanya jambo lisilo sahihi na kuumiza hisia za rafiki zake.

Saints, 1:97

Joseph Smith akitafakari kitandani.

Joseph alitaka watu kutafuta ufunuo kwa ajili ya maisha yao wenyewe. Lakini ingekuwa ya kutatiza kama kila mtu angejaribu kupata ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote.

Saints, 1:97

Joseph akishiriki ufunuo pamoja na Oliver Cowdery.

Hatimaye, Bwana alimpa Joseph ufunuo wa kushiriki na Oliver. Bwana alisema kwamba ni nabii pekee anayeweza kupokea ufunuo na amri kwa ajili ya Kanisa zima. Alisema kwamba Oliver anapaswa kufundisha hili kwa Hiram.

Mafundisho na Maagano 28: 2, 6-13.

Oliver akishiriki ufunuo kwa Hiram Page.

Bwana alimtaka Hiram kuelewa kwamba yeye angeweza kupokea ufunuo kwa ajili ya maisha yake mwenyewe. Lakini ufunuo kwa ajili ya Kanisa ungekuja kwa nabii wa Bwana. Hiram alimsikiliza Oliver na alitubu. Watakatifu sasa walielewa vyema jinsi Bwana anavyoliongoza Kanisa Lake.

Saints, 1:98