Hadithi za Maandiko
Lucy Morley na Familia Yake


“Lucy Morley na Familia Yake,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Lucy Morley na Familia Yake,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Novemba 1830

Lucy Morley na Familia Yake

Wengi wanaamini na kubatizwa

Lucy Morley akiwaalika wamisionari watatu katika nyumba ya Abigail Daniels.

Siku moja, Lucy Morley mwenye umri wa miaka 15 alikuwa akimsaidia jirani yake, Abigail Daniels, kufuma nguo. Walipokuwa wakifanya kazi, walisikia hodi mlangoni. Walikuwa ni wamisionari watatu. Abigail aliwakaribisha waingie ndani. Walisema kwamba Yesu Kristo alikuwa amewatuma kushiriki ujumbe.

Saints, 1:102–3

Wamisionari wakiwafundisha Lucy na Abigail kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Wanaume wale waliwaambia Abigail na Lucy kwamba Yesu alikuwa amemwita Joseph Smith kuwa nabii. Pia waliwaambia kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Saints, 1:103

Abigail akiwafanya wamisionari waondoke nyumbani kwake.

Kwa mshangao wa Lucy, Abigail alikasirika. Aliwafukuza wamisionari kuondoka nyumbani kwake.

Saints, 1:103

Lucy akiwaomba wale wamisionari kuitembelea familia yake.

Lucy alijua wamisionari hawa walikuwa watumishi wa Mungu. Aliwaambia waitembelee familia yake inayoishi mtaaa unaofuata. “Baba yangu anaishi maili moja kutoka hapa,” alisema. “Nendani huko na mtalishwa na kutunzwa.”

Saints, 1:103–4

Wamisionari wanashiriki mlo pamoja na Lucy na familia yake.

Lucy alikuwa sahihi. Wamisionari walipata chakula kizuri katika shamba la familia ya Morley. Wazazi wa Lucy walikuwa marafiki wa Sidney Rigdon. Waliamini Yesu aliwataka kushiriki kila kitu walichokuwa nacho kwa wengine. Waliwaalika wamisionari kuwafundisha wao na marafiki zao.

Saints, 1:104

Lucy, Abigail, na wengine wakibatizwa.

Usiku ule, majira ya usiku wa manane, watu 17 walibatizwa. Katika siku chache zilizofuata, watu 50 zaidi walikuja kwenye shamba la Morley kuwasikiliza wamisionari, na wakaomba kubatizwa. Hata rafiki yake Lucy Abigail Daniels alibadilisha mawazo yake kuhusu wamisionari. Yeye na mumewe waliamua kujiunga na Kanisa.

Saints, 1:105; Mafundisho na Maagano 20:25, 37