Hadithi za Maandiko
Joseph na Sidney Wanajifunza kuhusu Mbingu


“Joseph na Sidney Wanajifunza kuhusu Mbingu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Joseph na Sidney Wanajifunza kuhusu Mbingu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Februari 1832

Joseph na Sidney Wanajifunza kuhusu Mbingu

Ono kuhusu baraka za Mungu kwa watoto Wake

Joseph Smith na Sidney Rigdon wakisoma na kuijadili Biblia

Siku moja Joseph Smith na Sidney Rigdon walikuwa wakisoma Biblia. Walisoma kuhusu kile kinachotokea kwa watu baada ya kufa. Joseph na Sidney walifikiria kuhusu kile walichosoma, na walitaka kujifunza zaidi.

Mafundisho na Maagano 76:11–18

Joseph na Sidney wakiwa na ono la Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wamezungukwa na malaika.

Bwana aliwapa ono la kupendeza. Waliwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wakiwa wamezungukwa na malaika. Na walikuwa wamesikia sauti ikisema kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Sauti ilisema kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu na kisha akafufuka—Yeye alirudiwa na uhai. Kwa sababu Yeye alifufuka, sisi pia tutafufuliwa.

Mafundisho na Maagano 76:19–24, 39–43

Joseph na Sidney wakiwa na ono la ufalme wa telestia.

Joseph na Sidney walijifunza kwamba baada ya sisi kufufuka, tutaishi katika moja ya sehemu tatu huko mbinguni, zinazoitwa falme. Watu ambao hawakubali injili ya Yesu Kristo watakwenda kwenye ufalme wa telestia. Bwana alifananisha ufalme huu na mwangaza wa nyota.

Mafundisho na Maagano 76:81–86

Joseph na Sidney wakiwa na ono la ufalme wa terestria.

Joseph na Sidney pia walijifunza kuhusu ufalme unaoitwa ufalme wa terestria. Ufalme huu ni kwa ajili ya watu wanaoishi maisha mema lakini hawatii kikamilifu injili ya Yesu Kristo. Hawako imara katika imani yao Kwake. Bwana alilinganisha ufalme huu na mwangaza wa mwezi.

Mafundisho na Maagano 76:71–80

Joseph na Sidney wakiwa na ono la ufalme wa selestia.

Ufalme wa juu zaidi ni ufalme wa selestia Watu katika ufalme huu walifanya maagano, au ahadi, na Mungu na kushika maagano yao. Walitubu na kumfuata Yesu Kristo. Wanaishi na Baba wa Mbinguni na Yesu milele na kuwa kama Wao. Bwana alilinganisha ufalme huu na mwangaza wa jua.

Mafundisho na Maagano 76:50–70

Sidney akiandika kuhusu ono.

Bwana aliwaambia Joseph na Sidney wasishiriki kila kitu walichokiona katika ono lao. Lakini aliwataka waandike kuhusu baadhi yake na kushiriki na wengine. Waumini wengi wa Kanisa walikuwa na shauku ya kuwaambia watu kuhusu ono hilo.

Mafundisho na Maagano 76:113–119; Saints, 1:149–50

Watu wakisoma maelezo ya ono.

Baadhi ya watu hawakulipenda ono. Ilikuwa tofauti na kile walichoamini. Lakini wengi wa Watakatifu walikuwa na shukrani kujua kuhusu ufunuo huu. Uliwaonyesha kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake na aliwatengenezea njia ya kurudi Kwake.

Saints, 1:149–50