“Ujenzi wa Hekalu la Kirtland,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Ujenzi wa Hekalu la Kirtland,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Desemba 1832–Machi 1836
Ujenzi wa Hekalu la Kirtland
Nyumba maalumu kwa ajili ya Bwana
Bwana aliwaambia Joseph Smith kwamba ulikuwa wakati wa Watakatifu kujenga nyumba maalumu katika Kirtland. Nyumba hii itakuwa hekalu, mahali ambapo Bwana angewatembelea watu Wake na kufanya ahadi nao. Yeye angewapa zawadi maalum katika hekalu Lake. Yeye aliita zawadi hiyo endaumenti ya nguvu.
Mafundisho na Maagano 88:119; 95:8; Saints, 1:205
Watakatifu hawakuanza kujenga hekalu mara moja. Miezi michache baadaye, Bwana aliwakumbusha kwamba hekalu lilikuwa muhimu sana. Hyrum Smith alikimbilia nyumbani kwa wazazi wake kukusanya vifaa. Wakati mama yake alipomuuliza anaenda wapi, alisema alitaka kuwa wa kwanza kufanya kazi kwenye nyumba ya Bwana.
Watakatifu katika Kirtland walianza kujenga hekalu. Iligharimu pesa nyingi na ilichukua kazi nyingi. Waumini wa Kanisa kama Sidney Rigdon walitoa pesa nyingi kujenga hekalu. Walikuwa na shauku ya kufuata amri za Bwana na kupokea baraka Zake katika nyumba Yake.
Saints, 1:209–211
Watakatifu walipokuwa wakifanya kazi hekaluni, walianza kuishiwa pesa. Sidney na viongozi wengine wa Kanisa walikuwa na wasiwasi. Sidney alisali kwa Mungu kwa ajili ya msaada.
Saints, 1:210–11
Muumini wa Kanisa aliyeitwa Caroline Tippets na familia yake walikuwa wamehifadhi pesa nyingi. Caroline aliruhusu Kanisa kuazima fedha zao ili kusaidia kujenga hekalu.
Saints, 1:211–13
Watakatifu wengi katika Kirtland walifanya kazi kwa bidii ili kujenga hekalu. Baadhi waliendesha magari ya kukokotwa na maksai yaliyojaa mawe kwenda hekaluni. Wengine walitengeneza nguo na chakula kwa ajili ya wafanyakazi. Watoto walikusanya vipande vya vioo viliyovunjika ili kusaga na kuweka kwenye kuta za hekalu ili viweze kuangaza na kung’ara katika mwanga wa jua.
Saints, 1:210, 219, 221
Punde hekalu lilipomalizika! Watakatifu walikuwa na shauku ya kuingia ndani ya nyumba ya Bwana ili kupokea baraka alizowaahidi.
Saints, 1:221