“Misheni kwa Waamerika Wenyeji,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Misheni kwa Waamerika Wenyeji,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Oktoba 1830–Januari 1831
Misheni kwa Waamerika Wenyeji
Wahindi wa Delaware wanasikia injili
Mara baada ya Parley Pratt kubatizwa, Bwana alimwita kuungana na Oliver Cowdery na wengine katika misioni. Aliwataka wahubiri injili kwa Waamerika Wenyeji. Wamisionari walisafiri kwa wiki nyingi kupitia theluji nyingi. Hatimaye, walikutana na Kikthawenund, chifu wa Wahindi wa Delaware.
Mafundisho na Maagano 28:14; 30:5–6; 32; Saints, 1:98, 115
Chifu alikuwa rafiki kwa wamisionari. Aliwaalika marafiki zake kusikia ujumbe wao. Oliver alisema yeye na Parley walikuwa wamesafiri umbali mrefu ili kuwaletea Kitabu cha Mormoni. Kitabu hicho kinasimulia juu ya watu ambao waliishi katika mabara ya Amerika miaka mingi iliyopita. Mungu aliwataka kushiriki kitabu hicho ili kila mtu aweze kujua kuhusu Yesu Kristo.
Saints, 1:115-16
Oliver alimpatia Kikthawenund nakala ya Kitabu cha Mormoni. Alikuwa mwenye shukrani kwamba Oliver na marafiki zake walikuwa wamekuja kutoka mbali sana kushiriki Kitabu cha Mormoni kwa watu wake. Aliwaambia Oliver na Parley kwamba aliwataka warudi kuwasomea na kuwafundisha zaidi kuhusu Kitabu cha Mormoni.
Saints, 1:116–17