Hadithi za Maandiko
Joseph na Oliver Wanapokea Funguo za Ukuhani


“Joseph na Oliver Wanapokea Funguo za Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Joseph na Oliver Wanapokea Funguo za Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Aprili 1836

Joseph na Oliver Wanapokea Funguo za Ukuhani

Yesu Kristo na malaika wanatembelea Hekalu la Kirtland

Joseph Smith akipitisha sakramenti kwa Watakatifu katika Hekalu la Kirtland.

Wiki moja baada ya Hekalu la Kirtland kuwekwa wakfu, Watakatifu elfu moja walikutana hekaluni ili kumwabudu Mwokozi. Ilikuwa Jumapili ya Pasaka. Joseph Smith, Oliver Cowdery, na Mitume Kumi na Wawili walitoa sakramenti kwa Watakatifu.

Mafundisho na Maagano 110, kichwa cha habari cha sehemu; Saints, 1:239

Joseph Smith na Oliver Cowdery wakisali katika Hekalu la Kirtland.

Baada ya sakramenti, Joseph na Oliver walipata sehemu tulivu hekaluni, nyuma ya pazia, ili kusali.

Mafundisho na Maagano 110, kichwa cha habari cha sehemu; Saints, 1:239

Yesu Kristo akiwatokea Joseph na Oliver.

Walipomaliza kusali, waliangalia juu. Yesu Kristo alikuwa amesimama mbele yao! Yeye alijua Watakatifu walikuwa wamefanya kazi kwa bidii ili kujenga hekalu. “Nimeikubali nyumba hii,” Yeye alisema. Yesu aliwaambia Joseph na Oliver kwamba baraka za hekalu zingeleta shangwe kuu kwa watu wengi.

Mafundisho na Maagano 110:1–10

Musa akiwatokea Joseph na Oliver

Baada ya Yesu kuondoka, nabii Musa wa Agano la Kale aliwatokea Joseph na Oliver. Yeye aliwapa funguo za ukuhani za kukusanya Israeli. Hii ilimaanisha kwamba wangeweza kuongoza kazi ya kushiriki injili. Wangeweza kuwatuma wamisionari ulimwenguni kote kuwaleta watu katika Kanisa la Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 110:11

Elia akiwatokea Joseph na Oliver.

Kisha, nabii Elia alitokea. Aliwapa Joseph na Oliver funguo za kurejesha agano la Ibrahimu. Hii ilimaanisha kwamba Watakatifu wangeweza kupokea kutoka kwa Bwana agano lile lile Ibrahimu alilopokea. Wangekuwa na uwezo wa kuleta injili na baraka za Mungu kwa watu kila mahali kwa miaka mingi ijayo.

Mafundisho na Maagano 110:12

Eliya aliwatokea Joseph na Oliver

Hatimaye, nabii Eliya alitokea. Aliwapa Joseph na Oliver funguo za ukuhani kufunga, au kuunganisha, familia milele. Kazi ambayo Watakatifu walifanya katika mahekalu ingekubaliwa mbinguni. Sasa Kanisa lilikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Mwokozi na kujiandaa kwa ajili Yake kuja duniani tena.

Mafundisho na Maagano 110:13–16