Hadithi za Maandiko
Lulu ya Thamani Kuu


“Lulu ya Thamani Kuu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Lulu ya Thamani Kuu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Julai 1835–Machi 1842

Lulu ya Thamani Kuu

Maandiko zaidi kutoka kwa Bwana

Joseph Smith akiangalia ya hati ndefu ya kukunja ya Kimisri.

Siku moja, mtu alikuja Kirtland na mumiani kutoka Misri. Pamoja na mumiani kulikuwa na hati ndefu za kukunja, au misokoto ya karatasi ya zamani. Hati hizo ndefu za kusokotwa zilikuwa na maandishi ya Kimisri. Mtu yule aliyaonyesha kwa Nabii Joseph Smith. Joseph alivutiwa sana na maandishi yale.

Saints, 1:219–20

Joseph akishiriki hati hizo ndefu za kukunja pamoja na Emma Smith.

Baadhi ya marafiki walimsaidia Joseph kununua mumiani na hati hizo za kukunjwa. Wakati Joseph akiyasoma maandishi yale, Bwana alimfunulia maandishi ya kale kutoka kwa Ibrahimu, nabii katika Biblia. Kwa msaada kutoka kwa marafiki kama Oliver Cowdery, Joseph aliandika kile Bwana alichomfundisha kuhusu mafundisho ya Ibrahimu.

Saints, 1:220

Joseph akiwa na ono la Ibrahimu na Baba wa Mbinguni.

Ibrahimu alikuwa ameona ono la maisha yetu na Baba wa Mbinguni kabla hatujazaliwa. Aliona kwamba Yesu alichaguliwa kuwa Mwokozi wetu. Ibrahimu pia alijifunza kuhusu uumbaji wa ulimwengu. Watakatifu walifurahia kuwa na mafundisho haya kutoka kwa Ibrahimu. Walikuwa na furaha Bwana alitaka kuwafundisha zaidi.

Ibrahimu 2:6–11; 3–5; Saints, 1:220

Joseph akipokea mwongozo wa kiungu kutoka kwenye hadithi za Musa na Ibrahimu.

Maandishi ya Ibrahimu yakawa sehemu ya kitabu cha maandiko kilichoitwa Lulu ya Thamani Kuu. Kitabu hiki pia kina maandishi kutoka kwa Musa, nabii mwingine katika Biblia. Yanafundisha kweli ambazo zinakosekana kutoka kwenye Biblia. Bwana alitaka watu wajue kweli hizi, kwa hivyo Yeye alizishiriki na Joseph Smith.

Musa 1–8; Ibrahimu 1–5

Mvulana na msichana wakisoma Lulu ya Thamani Kuu.

Lulu ya Thamani Kuu pia inao ushuhuda wa Joseph Smith na Makala za Imani 13. Joseph Smith aliandika mambo haya ili kuuambia ulimwengu kile ambacho Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini. Lulu ya Thamani Kuu ni kitabu kidogo, kama lulu ilivyo kidogo, lakini ni cha thamani sana.

Joseph Smith—Historia; Makala ya Imani 1