Hadithi za Maandiko
Parley na Thankful Pratt


“Parley na Thankful Pratt,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Parley na Thankful Pratt,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Agosti–Septemba 1830

Parley na Thankful Pratt

Imani ya kumfuata Roho

Parley na Thankful Pratt kwenye shamba lao.

Parley Pratt na Thankful Pratt walikuwa wakulima huko Ohio. Siku moja, Parley alihisi Roho akimwambia aondoke nyumbani kwake aende kuwafundisha watu kuhusu Biblia.

Saints, 1:92

Parley na Thankful wakiondoka kwenda kufundisha kuhusu Biblia.

Parley na Thankful waliuza shamba lao. Hawakujua wapi wangeenda, lakini waliamini kwamba Mungu angewabariki kwa kumtumikia Yeye.

Saints, 1:92

Parley akitoka nje ya boti huko New York.

Parley na Thankful walichukua baadhi ya nguo na pesa na kwenda kuingia kwenye boti. Walipokuwa wakisafiri kupita New York, Roho alimwambia Parley kushuka kwenye boti hiyo. Parley alimwambia Thankful kuendelea bila yeye. Aliahidi angeungana naye karibuni. Alihisi kulikuwa na kitu ambacho Mungu alimtaka afanye huko New York.

Saints, 1:92

Parley akijifunza kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Parley alitembea kwa mwendo mrefu. Hatimaye alifika nyumbani kwa mhubiri. Mhubiri alimwambia Parley kuhusu kitabu kigeni ambacho mtu alikuwa amempatia. Kimetokea kwenye mabamba ya dhahabu na kiliandikwa zamani sana. Kiliitwa Kitabu cha Mormoni. Mvulana huko New York alikuwa amekitafsiri kwa nguvu za Mungu.

Saints, 1:92

Parley akipokea ushuhuda juu ya Kitabu cha Mormoni.

Parley alikuwa mdadisi sana. Mhubiri alimwonyesha Parley hicho kitabu. Akiwa mwenye kusisimuka, Parley akakifungua na kuanza kusoma. Masaa yalipita, lakini hakuweza kuacha kusoma, hakuweza hata kula wala kulala. Roho wa Bwana alimwambia kilikuwa cha kweli.

Saints, 1:92–93

Parley na Hyrum Smith wakizungumza kuhusu Kitabu cha Mormoni.

Parley alikipenda sana Kitabu cha Mormoni, alitaka kumpata mtu aliyekitafsiri. Alitembea kwenda kwenye shamba la familia ya Smith, ambapo alikutana na Hyrum, kaka yake Joseph. Walizungumza usiku wote. Hyrum alimwambia Parley kwamba Kitabu cha Mormon ni cha kweli. Alimpatia Parley nakala yake mwenyewe ya hicho kitabu.

Saints, 1:93

Parley akiendelea kusoma Kitabu cha Mormoni.

Alipoendelea kusoma, Parley alijifunza kwamba Yesu Kristo alikuwa amewatembelea watu katika mabara ya Amerika miaka mingi iliyopita. Parley aliweza kuona kwamba Kitabu cha Mormoni kilikuwa na thamani zaidi ya utajiri wote wa ulimwengu. Hakuweza kusubiri kurudi kwa Thankful na kushiriki naye kile alichojifunza.

, 1:93; 3 Nefi 11:1–12

Parley akishiriki Kitabu cha Mormoni kwa Thankful na familia yake.

Parley aliwaambia Thankful na wanafamilia wake kuhusu Kitabu cha Mormoni. Aliwaambia kile ambacho kitabu hufundisha kuhusu Yesu Kristo. Thankful alifurahi kwamba Parley alikuwa amemfuata Roho na kupata kazi ambayo Mungu alitaka yeye afanye. Kama Parley, Thankful alijifunza mwenyewe kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.

Saints, 1:98–99