“Siku ya Uponyaji,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Siku ya Uponyaji,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
Aprili–Julai 1839
Siku ya Uponyaji
Kubariki wagonjwa kwa nguvu za Mungu
Wakati Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa walipokuwa wafungwa huko Missouri, baadhi ya walinzi waliwapeleka katika gereza tofauti. Walinzi walikuwa wakarimu kwa wale wafungwa. Usiku mmoja, kiongozi wa walinzi alimwambia Joseph yeye alikuwa anaenda kulala, na kama Joseph na marafiki zake watatoroka, yeye asingewazuia.
Saints, 1:392–93
Joseph na viongozi wengine wa Kanisa walitoroka. Walikuta familia zao zikiishi katika mji ulioitwa Quincy.
Saints, 1:395–96
Watu waliokuwa Quincy walikuwa wakarimu kwa Watakatifu. Waliwapatia Watakatifu chakula na nguo na mahali pa kukaa.
Saints, 1:377
Watakatifu walikuwa na shukrani kwa ukarimu wa watu wa Quincy. Lakini Joseph alijua wangehitaji sehemu zao wenyewe za kuishi. Viongozi wa Kanisa walinunua ardhi ambayo hakuna mtu mwingine aliyeitaka, na Watakatifu walianza kuhamia huko.
Saints, 1:399-400
Nchi ilikuwa karibu na mto mkubwa. Ilikuwa ardhi oevu na yenye matope na iliyoojaa mbu. Mbu waliwafanya Watakatifu wengi kuwa wagonjwa sana na ugonjwa unaoitwa malaria. Baadhi yao walikufa.
Saints, 1:402
Wakati Joseph alipoona kwamba watu wengi walikuwa wagonjwa, aliwakusanya baadhi ya viongozi wa Kanisa na kuwaomba waongozane naye. Asubuhi yote, walikwenda kutoka familia moja hadi familia nyingine, wakiwatembelea watu wagonjwa na kuwabariki. Walitumia nguvu za Yesu Kristo kuwaponya magonjwa yao.
Saints, 1:402
Mtu mmoja waliyemtembelea alikuwa Elijah Fordham. Alikuwa mgonjwa sana, mkewe alifikiri angekufa hivi karibuni. Joseph alimwuliza Elijah kama alikuwa na imani ya kuponywa.
Saints, 1:402
Elijah alisema, “Ninaogopa nimechelewa sana.” Joseph alimuuliza Elijah kama alimwamini Yesu Kristo. “Ndiyo ninaamini, Kaka Joseph,” yeye alijibu.
Saints, 1:402
Joseph alimbariki katika jina la Yesu Kristo. Elijah alisimama. Yesu alikuwa amemponya! Elijah kisha alimfuata Joseph kwenye nyumba iliyofuata na kumsaidia kubariki watu wengine ambao walikuwa wagonjwa.
Saints, 1:402–3