Hadithi za Maandiko
Sidney na Phebe Rigdon


“Sidney na Phebe Rigdon,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Sidney na Phebe Rigdon,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Oktoba–Novemba 1830

Sidney na Phebe Rigdon

Wanabadilisha maisha yao ili kuikubali injili

Parley Pratt akipendekeza kwa wenzake kwamba wamtembelee rafiki yake Sidney.

Parley Pratt na wengine walikuwa wanakwenda kushiriki injili na Waamerika Wenyeji. Wakiwa njiani, Parley alitaka kusimama na kumtembelea rafiki yake Sidney Rigdon. Sidney alikuwa mhubiri ambaye alikuwa amemfundisha Parley kuhusu Yesu Kristo katika Biblia. Sasa Parley alitaka kumfundisha Sidney kuhusu Yesu katika Kitabu cha Mormoni.

Mafundisho na Maagano 32; Saints, 1:99

Parley akishiriki Kitabu cha Mormoni kwa Sidney Rigdon.

Parley alimwambia Sidney kuhusu Kitabu cha Mormoni na kumwalika akisome. Sidney hakuwa na uhakika, lakini kwa sababu Parley alikuwa rafiki, aliahidi angefanya hivyo.

Saints, 1:100

Sidney akisoma Kitabu cha Mormoni na kukishiriki na mkewe.

Wakati Sidney aliposoma Kitabu cha Mormoni, alijua kilitoka kwa Mungu. Alishiriki hisia zake kwa mkewe, Phebe.

Saints, 1:101

Sidney akizungumza na familia yake.

Lakini Sidney hakuwa na uhakika wa nini cha kufanya baada ya hilo. Kama angebatizwa, angepoteza kazi yake kama mhubiri katika kanisa lake. Ni kwa jinsi gani angeweza kuwatunza Phebe na watoto wao sita? Watu katika kanisa lake wangejisikiaje? Aliomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya msaada, na akawa na hisia ya amani.

Sainta, 1:101; Mafundisho na Maagano 19:23

Phebe Rigdon akimwambia Sidney kwamba yuko tayari kujiunga na Kanisa.

Sidney alimuuliza Phebe kama alikuwa tayari kuacha maisha yao ya starehe na kujiunga na kanisa hili jipya pamoja naye. “Ni tamanio langu kufanya mapenzi ya Mungu,” alisema, “iwe katika uzima au kifo.” Waliamua kubatizwa.

Saints, 1:101

Sidney anakutana na Joseph Smith.

Baadaye, Sidney alikutana na Nabii Joseph Smith. Bwana alimpa Sidney ujumbe kupitia Joseph. Alisema kwamba alikuwa ameona vitu vizuri ambavyo Sidney alikuwa amefanya na kusikia sala zake. Bwana alimwambia Sidney Yeye alikuwa na kazi kubwa ya yeye kufanya. Sidney angefanya mambo makubwa.

Mafundisho na Maagano 35:3–4