“Susa Young Gates na Joseph F. Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Susa Young Gates na Joseph F. Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
1902–1918
Susa Young Gates na Joseph F. Smith
Ufunuo kuhusu ulimwengu wa roho
Susa Young Gates alikuwa binti wa Brigham Young. Alizaliwa Utah na kukulia huko. Alipenda kuandika, na alipenda kuhudumu katika Kanisa la Bwana.
Saints, 3:9–10, 64
Wakati Susa alipokuwa mtu mzima, aliugua sana. Aliomba baraka ya ukuhani. Katika baraka, Bwana alimwambia Susa Yeye alimtaka afanye kazi ya hekalu.
Saints, 3:193–94
Baada ya baraka, Susa alijisikia vizuri. Alitumia muda wake kujifunza kuhusu historia ya familia yake. Alipowapata wanafamilia waliofariki bila kubatizwa, alikwenda hekaluni kubatizwa kwa niaba yao. Alipenda kuwaambia watu kuhusu kazi ya historia ya familia. Kwa huzuni, watu wengi hawakupendezwa.
Saints, 3:194–95, 206
Siku moja, Susa alimtembelea rafiki yake Joseph F. Smith, Rais wa Kanisa. Rais Smith alikuwa mgonjwa kwa wiki nyingi. Susa alijua kwamba alikuwa na huzuni sana kwa sababu mwanawe alikuwa amefariki. Alikuwa na huzuni kuhusu mambo mengine yanayotokea ulimwenguni pia, kama vita na magonjwa.
Saints, 3:197–99, 205–6
Lakini Susa alipoketi chini na Rais Smith, alifurahi kuzungumza naye. Alimwambia Susa kwamba Mungu amempa ono maalum. Ilikuwa yote kuhusu ulimwengu wa roho, ambapo watu huenda baada ya kufariki. Ono lake liliandikwa kwenye karatasi. Rais Smith alimpa Susa na kumuomba asome.
Saints, 3:206–7
Susa alisoma karatasi ile. Ilisema kwamba Yesu Kristo alitembelea ulimwengu wa roho. Alimtuma Adamu, Hawa, na wanaume na wanawake wengine waaminifu kufundisha roho ambao hawakupokea injili walipokuwa hai. Walikuwa wakisaidia roho hizi kujiandaa ili watu waweze kubatizwa kwa niaba yao hekaluni.
Mafundisho na Maagano 138:11–19, 29–48; Saints, 3:206–7
Susa alishangazwa aliposoma ono la Rais Smith. Rais Smith alitabasamu kwake. “Susa,” alisema, “utafanya kazi kubwa.” Alimwambia kwamba alimpenda kwa ajili ya imani yake katika Bwana.
Saints, 3:206
Susa aliandika kuhusu ufunuo katika shajara yake. “Ee, ilikuwa faraja kwangu!” alisema. Hakuweza kungoja kuwaambia rafiki zake na waumini wengine wa Kanisa kuhusu hilo. Alijua ono la Rais Smith lingewasaidia Watakatifu kufurahia kufanya kazi ya hekaluni kwa watu katika ulimwengu wa roho.
Saints, 3:207