Hadithi za Maandiko
Samuel Smith Anashiriki Kitabu cha Mormoni


“Samuel Smith Anashiriki Kitabu cha Mormoni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Samuel Smith Anashiriki Kitabu cha Mormoni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

1830–1832

Samuel Smith Anashiriki Kitabu cha Mormoni

Kitabu kimoja kinabariki maisha ya wengi

Samuel Smith akishiriki Kitabu cha Mormoni na John na Rhoda Greene.

Bwana alimwita Samuel Smith, kaka mdogo wa Joseph, katika misheni ya kushiriki injili. Samweli alikutana na John na Rhoda Greene na kuwaambia kuhusu Kitabu cha Mormoni. John alikuwa mhubiri katika kanisa lingine. Alisema kwamba atachukua nakala ya kitabu na kuona kama mtu yeyote katika kanisa lake alitaka kukisoma.

Saints, 1:99

Rhoda akimrudishia Samweli Kitabu cha Mormoni.

Baada ya miezi michache, Samweli alirudi. Rhoda alisema mumewe hakuweza kumpata mtu yeyote aliyetaka kusoma Kitabu cha Mormoni. Alimrudishia Samweli.

Saints, 1:99

Rhoda akimwambia Samweli kwamba alipenda kusoma Kitabu cha Mormoni.

Samuel alihuzunika. Aligeuka kuondoka, lakini Rhoda alimsimamisha. Alisema kwamba alikuwa amesoma Kitabu cha Mormoni, na alikipenda.

Saints, 1:99

Samweli akimrudishia Rhoda Kitabu cha Mormoni na kumwalika kumwomba Mungu kwa ajili ya ushuhuda.

Roho Mtakatifu alimwambia Samweli arudishe kitabu hicho kwa Rhoda. “Muombe Mungu akupe ushuhuda,” Samweli alimwambia. Alimfundisha Rhoda kuhusu Roho Mtakatifu na jinsi ambavyo angejua kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.

Moroni 10:3–5; Saints, 1:99–100

Samuel akirudi nyumbani kutoka kwenye misheni yake.

Samweli alirudi nyumbani kutoka kwenye misheni yake. Hakuwa amembatiza mtu yeyote, na watu wachache tu walipendezwa na Kitabu cha Mormoni.

Rhoda akishiriki Kitabu cha Mormoni na kaka yake, Brigham Young.

Rhoda na John waliomba, na Roho Mtakatifu aliwaambia Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Kisha Rhoda alishiriki kitabu hicho na kaka yake, Brigham Young.

Saints, 1:100

Brigham Young na Heber Kimball wakisoma Kitabu cha Mormoni.

Brigham na rafiki yake, Heber Kimball, walikuwa wakitafuta Kanisa la kweli la Yesu. Walikisoma Kitabu cha Mormoni. Walijifunza na kusali kuhusu injili ya Yesu Kristo kwa takribani miaka miwili.

Brigham akimsikiliza mmisionari akitoa ushuhuda wake.

Wakati huu, Brigham na Heber walikwenda kwenye mikutano ya Kanisa pamoja na familia zao. Katika mojawapo ya mikutano hii, Brigham alimsikia mmisionari akishiriki ushuhuda wake. Mmisionari hakuwa mnenaji mzuri, lakini Brigham alihisi Roho Mtakatifu wakati mmisionari alipokuwa akizungumza. Brigham alijua alikuwa anasema ukweli.

Brigham na Heber wakishiriki injili.

Brigham, Heber, na wake zao, Miriam na Vilate, walibatizwa. Walimpenda Mwokozi na injili Yake. Miaka kadhaa baadaye, Bwana alimwita Brigham na Heber kuwa Mitume Wake na kuhudumu misheni. Kwa sababu Samweli alishiriki Kitabu cha Mormoni, watu wengi walijiunga na Kanisa la Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 124:127–29; 126; Saints, 1:215–16