Hadithi za Maandiko
Kukusanyika Ohio


“Kukusanyika Ohio,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Kukusanyika Ohio,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Desemba 1830–Mei 1831

Kukusanyika Ohio

Imani ya Lucy Smith na muujiza

Lucy Smith na wanafamilia wakijiandaa kuhamia Ohio.

Huko Ohio, watu wengi zaidi na zaidi walikuwa wakijiunga na Kanisa. Bwana aliwaambia Joseph Smith kwamba Watakatifu wanaoishi katika maeneo mengine wanapaswa kukusanyika Ohio. Ingeweza kuwa safari ndefu. Lakini Bwana aliahidi kwamba baada ya kukusanyika, Yeye angewafundisha Watakatifu sheria Yake na kuwabariki kwa uwezo wa kufanya kazi Yake.

Mafundisho na Maagano 37; 38:32; Saints, 1:109–110

Lucy na wasafiri wengine wakiingia ndani ya mashua kwenda Ohio.

Mama yake Joseph, Lucy, na kundi la takriban waumini wa Kanisa 80 waliacha nyumba zao huko New York na kuhamia Ohio. Walipanda kwenye mashua ambayo ingewabeba sehemu ya safari. Baada ya kusafiri kwa siku chache, mashua ilibidi isimame. Barafu nene ndani ya maji ilizuia njia yao.

Saints, 1:121–22

Mashua inazuiliwa na barafu ndani ya bandari.

Watakatifu iliwabidi wasubiri barafu ivunjike vipande. Walikuwa wamechoka, walikuwa na njaa, walilowana na wenye kuona baridi.

Saints, 1:122

Baadhi ya Watakatifu wakikosa subira na kuanza kubishana.

Ilikuwa ni vigumu kusubiria. Baadhi ya Watakatifu walianza kubishana wao kwa wao.

Saints, 1:122

Lucy akiwaambia Watakatifu kuomba kwa Mungu ili aivunje barafu ndani ya bandari.

Lucy hakupenda kuwasikia Watakatifu wakibishana. Alijua alihitaji kusema kitu. “Imani yenu iko wapi?” aliuliza. Lucy aliwaambia Watakatifu kwamba kama wangeomba kwa Mungu, Yeye angevunja barafu ili waweze kuendelea na safari yao.

Saints, 1:122–23

Njia inayofunguka ndani ya barafu.

Ghafla, walisikia kelele kama radi wakati barafu ilipovunjika. Njia ilifunguliwa ndani ya ile barafu, pana ya kutosha kwa ajili ya mashua yao kupita.

Saints, 1:123

Watakatifu wakikusanyika kumshukuru Baba wa Mbinguni.

Watakatifu walishangazwa na kuwa na shukrani. Walikusanyika kusali na kumshukuru Baba wa Mbinguni. Mashua yao ilisafiri salama kuelekea Ohio.

Saints, 1:123

Watakatifu wakikaribishwa Ohio.

Wakati Watakatifu walipofika Ohio, waumini wa Kanisa huko waliwakaribisha na kuwasaidia kupata sehemu za kuishi. Bwana alitimiza ahadi Yake kuwafundisha sheria Yake na kuwapa uwezo wa kufanya kazi Yake.

Mafundisho na Maagano 42; Saints, 1:126