Hadithi za Maandiko
Akina Knight na Wengine Wanakusanyika Sayuni


“Akina Knight na Wengine Wanakusanyika Sayuni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Akina Knight na Wengine Wanakusanyika Sayuni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Desemba 1830–Agosti 1831

Akina Knight na Wengine Wanakusanyika Sayuni

Kutii wito wa Bwana

Polly na Joseph Knight wakihamia Ohio na Watakatifu wengine.

Polly na Joseph Knight waliishi na familia yao huko New York. Walimjua Nabii Joseph vizuri. Baada ya kujifunza injili, walichagua kujiunga na Kanisa. Wakati Bwana alipowaomba Watakatifu kuhamia Ohio, akina Knight walitii.

Mafundisho na Maagano 37; Saints, 1:33, 94, 109–110

Leman Copley akiwasalimia Watakatifu huko Ohio.

Akina Knight walikuwa na furaha walipowasili Ohio. Leman Copley, muumini wa Kanisa, alisema baadhi ya Watakatifu wangeweza kuishi katika ardhi yake. Kulikuwa na nafasi ya kutosha ya kupanda mazao na kujenga nyumba. Joseph Knight na wanawe walifanya kazi kwa bidii ili kuyaandaa mashamba tayari kwa ajili ya kupanda.

Saints, 1:126–27

Watakatifu wakiondoka kwenye ardhi ya Leman Copley.

Lakini siku moja, Leman alibadilisha mawazo yake kuhusu ardhi yake. Hakutaka Watakatifu kuishi huko tena. Aliwaambia akina Knight na kila mtu mwingine waondoke.

Saints, 1:127

Watakatifu wakimwuliza Joseph Smith kile wanachopaswa kufanya.

Watakatifu walikuwa na wasi wasi. Sasa hawakuwa na mahali pa kuishi. Walimwuliza Nabii Joseph kile walichopaswa kufanya.

Mafundisho na Maagano 54; Saints, 1:127

Joseph akiwaambia Watakatifu kwenda Missouri kujenga Sayuni.

Bwana alisema kwamba Watakatifu hawa wanapaswa kwenda Missouri na kujenga Sayuni. Sayuni ingekuwa mji ambapo watu wa Bwana wangeweza kukusanyika. Katika Sayuni, wangejenga hekalu ambapo wangefanya maagano, au ahadi na Mungu. Yeye angewabariki kama wangeshika maagano haya. Akina Knight walikuwa na shauku ya kwenda huko.

Mafundisho na Maagano 29:1–8; 42:30–36; 45:59–66; 54:6–9; 57:1–2; Saints, 1:128

Familia ya Polly ikimtunza akiwa njiani kuelekea Missouri.

Wakati akina Knight waliposafiri kwenda Missouri, Polly akawa mgonjwa sana. Mume wake, Joseph, na wanawe walihofia kwamba hangeishi kwa muda mrefu zaidi. Lakini Polly aliiambia familia yake kwamba alitaka kuwa Sayuni kabla ya kufariki. Alitaka hivyo zaidi ya kitu kingine cho chote!

Saints, 1:128

Akina Knight wakiwasili Missouri.

Baada ya safari ndefu, Akina Knight waliwasili Missouri. Polly alikuwa na shukrani sana kwa Bwana kwamba alikuwa ameishi kuiona. Akina Knight walidhani nchi ilikuwa nzuri. Walikuwa na imani kwamba wangeweza kutii amri ya Bwana ya kujenga Sayuni huko.

Saints, 1:132

Watakatifu wakiweka jiwe kuweka alama mahali ambapo hekalu jipya litakuwa.

Watakatifu walisema sala maalum na kuiita ardhi hiyo Sayuni, ambapo watu wa Bwana wangekuja. Nabii Joseph aliweka jiwe ili kuweka alama mahali ambapo kona ya hekalu ingekuwa. Siku chache baadaye, Polly alifariki. Bwana aliahidi kwamba Watakatifu walio kuja Sayuni na kufa wangepumzika mbinguni.

Mafundisho na Maagano 59:1–2; Saints, 1:132–33