Hadithi za Maandiko
Mashahidi Wanayaona Mabamba ya Kitabu cha Mormoni


“Mashahidi Wanayaona Mabamba ya Kitabu cha Mormoni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Mashahidi Wanayaona Mabamba ya Kitabu cha Mormoni,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

Machi–Septemba 1829

Mashahidi Wanayaona Mabamba ya Kitabu cha Mormoni

Kutoa ushuhuda kwa ulimwengu

Baadhi ya watu wa miji walikasirishwa na Joseph Smith.

Joseph, Emma, na Oliver waliendelea kutafsiri mabamba ya dhahabu nyumbani kwa Smith huko Pennsylvania. Lakini watu katika mji wao walitaka kuwazuia. Oliver alikuwa na rafiki aliyeitwa David Whitmer aliyeishi huko New York. Oliver alimwomba David kama wangeweza kuhamia kuishi pamoja na familia ya Whitmer ili kumalizia tafsiri.

Saints, 1:68

David Whitmer akimkaribisha Joseph, Emma, na Oliver nyumbani mwake.

David na familia yake walikubali. Waliwakaribisha Joseph, Emma, na Oliver katika nyumba yao. Sasa wangeweza kufanyia kazi tafsiri hiyo kwa amani. Kulikuwa na watu wengi walioishi katika nyumba ya Whitmer. Hiyo ilimaanisha kulikuwa na kazi nyingi za kufanya, hasa kwa mama wa David, Mary.

Saints, 1:68–70

Malaika Moroni akimtokea Mary Whitmer.

Siku moja, wakati Mary alipokuwa akifanya kazi, malaika Moroni alimtembelea. Alisema kwamba alijua kazi yote ya ziada ilikuwa inamfanya achoke. Alitaka kuimarisha imani yake. Alifungua mfuko na kuchomoa mabamba ya dhahabu. Aligeuza kurasa na kumwonyesha Mary maandishi. Alimuahidi Mary kwamba angebarikiwa.

Saints, 1:70–71

David Whitmer, Martin Harris, na Oliver Cowdery wakimuuliza Joseph kama wanaweza kuwa mashahidi.

Baadhi ya watu hawakuamini kwamba mabamba hayo yalikuwepo. Joseph alikuwa ametii amri ya Bwana ya kutoonyesha mabamba hayo kwa mtu yeyote. Bwana alisema angewaruhusu mashahidi watatu zaidi waone mabamba hayo. David Whitmer, Martin Harris, na Oliver Cowdery waliuliza kama wangeweza kuwa mashahidi. Bwana alisema wangeweza kuona.

Mafundisho na Maagano 5:11–12; 17; Saints, 1:73

Joseph, Martin, Oliver, na David wakiomba ili kupokea ushahidi wa mabamba ya dhahabu.

Joseph, Martin, Oliver, na David walikwenda msituni. Walipiga magoti na kufanya zamu kumwomba Mungu kama wangeweza kuona mabamba hayo, lakini hakuna kilichotokea.

Saints, 1:73

Martin Harris akiondoka kwenye kundi.

Martin Harris alihisi kwamba yeye alikuwa sababu ya maombi yao kutojibiwa. Martin aliondoka, na wengine waliendelea kusali.

Saints, 1:73

malaika anamtokea Oliver, David, na Joseph.

Kisha malaika akatokea katika nuru angavu. Aliwaonyesha Oliver na David mabamba ya dhahabu na maandishi juu yake. Walisikia sauti ya Mungu ikisema kwamba Joseph alikuwa ametafsiri mabamba kwa uwezo wa Mungu na kwamba tafsiri ilikuwa sahihi. Mungu pia alisema wanapaswa kumwambia kila mtu kile walichokuwa wameona na kusikia.

“Ushuhuda wa Mashahidi Watatu”; Saints, 1:73–74

malaika anawatokea Martin na Joseph.

Joseph alikwenda kumtafuta Martin. Alikuwa bado anasali. Joseph alisali pamoja naye. Kisha malaika akatokea na kumwonyesha Martin mabamba, kama vile alivyofanya kwa Oliver na David.

Saints, 1:74

Joseph anawaambia wazazi wake kwamba watu wengine wameyaona hayo mabamba ya dhahabu.

Kisha, Joseph alikwenda kuwatafuta wazazi wake, ambao walikuwa wakimtembelea Mary Whitmer. Aliwaambia jinsi alivyokuwa na furaha kwamba watu wengine walikuwa wameyaona hayo mabamba. Sasa mashahidi wangeweza kuwaambia watu kwamba Joseph alikuwa anasema ukweli. Martin alimwambia kila mtu jinsi alivyofurahi kwamba Mungu alimruhusu kuwa mmoja wa mashahidi.

Saints, 1:74–75

Watu wanane zaidi wanapokea ushahidi wa mabamba ya dhahabu.

Siku chache baadaye, Bwana alimwambia Joseph aonyeshe mabamba ya dhahabu kwa watu wengine wanane—baba yake, wawili kati ya kaka zake, kaka wanne wa David, na shemeji wa David. Walipata kushikilia yale mabamba na kugeuza kurasa zake. Walijua mabamba yalikuwa halisi.

Ushuhuda wa Mashahidi Wanane”; Saints, 1:75

Joseph na Martin wakiangalia muswada uliochapishwa.

Tafsiri ya Kitabu cha Mormoni sasa ilikuwa imekamilika. Joseph alimpa malaika Moroni yale mabamba ya dhahabu. Sasa ulikuwa wakati wa kuchapisha nakala za kitabu ili kila mmoja aweze kukisoma na kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.

Saints, 1:75–76

Joseph na Martin wakisherehekea kuchapishwa kwa Kitabu cha Mormoni.

Iligharimu pesa nyingi kuchapisha Kitabu cha Mormoni. Martin Harris alitoa sehemu ya shamba lake ili kulipia gharama zake. Alifanya hivi kwa sababu alijua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Kila nakala ya kitabu ina ushuhuda wa Martin na mashahidi wengine kwa ajili ya wote kusoma. Mashahidi hao kamwe hawakukana ushuhuda wao.

Mafundisho na Maagano 19:26–27, 34–35; Saints, 1:76–78