“Rais Timothy L. Farnes,” Liahona, Mei 2025.
Rais Timothy L. Farnes
Rais Mkuu wa Wavulana
Wakati Rais Timothy L. Farnes alipokuwa na umri wa miaka 14, rafiki wa imani nyingine alianza kupinga imani yake ya kidini. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ujana, Timothy alishuhudia kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu na kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni la kweli.
“Roho alijaa chumbani humo. Ilikuwa ya kuhisika,” alikumbuka. “Sote tulihisi hivyo, na sote tulibadilika.”
Rais Farnes alisema anataka vijana wa Kanisa wajue wao ni wa familia ya Mungu.
“Wao ni watoto wa Mungu na watoto wa agano,” alisema, “na wanaweza kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kama watamkubali Yeye—kukubali zawadi ambayo ni yao kwa sababu ya Upatanisho Wake.”
Timothy Lowell Farnes alizaliwa mnamo Juni 29, 1969, huko Baltimore, Maryland, kwa Gary William Farnes na Mary Ellen Farnes. Alipokuwa mtoto, familia yake ilihamia Utah, ambako alikulia. Yeye ni wa kwanza kati ya watoto saba.
Rais Farnes alihudumu kama mmisionari katika Misioni ya Brazil Porto Alegre. Alisomea uchumi katika Chuo Kikuu cha Brigham Young na baadaye alianzisha makampuni mengi, ikiwa ni pamoja na MedSource Direct, Aspire, na taasisi ya misaada ya kibinadamu isiyo ya faida ya World Joy.
Alimuoa Linsey Anne Farnes katika Hekalu la Salt Lake mnamo Agosti 27, 1992. Wana watoto watano na wajukuu sita, na wanaishi huko Bountiful, Utah.
Rais na Dada Farnes walihudumu kama viongozi wa misioni katika Misioni ya Brazil São Paulo North kuanzia mwaka 2014 hadi 2017. Miito iliyopita ya Rais Farnes inajumuisha Sabini wa Eneo katika Eneo la Utah, rais wa kigingi, mshiriki wa baraza kuu, askofu, na askofu wa vijana waseja.