2025
Mzee Brik V. Eyre
Mei 2025


“Mzee Brik V. Eyre,” Liahona, Mei 2025.

Mzee Brik V. Eyre

Sabini Mkuu mwenye Mamlaka

Mzee Brik V. Eyre anauita uzoefu wake wa kutumikia miaka mitatu kama rais wa Misioni ya Arizona Phoenix “usioweza kuaminika.”

Kuhusu kuhudumu pamoja na mke wake, Susan, yeye alisema, “Umefungwa nira sawa na mwenzi wako, … nasi tunatumikia bega kwa bega.” Na juu ya kuhudumu pamoja na mamia ya wamisionari, aliongeza, “Sijui kama ninaweza hata kuielezea baraka ya kupendeza ya kutumia kila siku na wawakilishi wenye mamlaka kutoka kwa Yesu Kristo kwa miaka mitatu.”

Brik Vern Eyre alizaliwa januari 17, 1964, huko Logan, Utah, kwa Vern Bingham Eyre na Emma Rae Anderson Eyre. Ana dada zakewatano wakubwa na mababu kadhaa miongoni mwa waumini wa mwanzo wa Kanisa.

Mzee Eyre alihudumu katika Misioni ya Guatemala City. Alimuoa Susan Zari Rahimzadeh katika Hekalu la Logan Utah mnamo Juni 27, 1987. Baba wa Dada Eyre ni wa ukoo wa Kiislamu, na mama yake ni wa ukoo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Akina Eyres, ambao walikuwa wakiishi Park City, Utah, wakati wa wito wao, wana watoto watano ambao kwa sasa ni watu wazima.

Mzee Eyre alipata shahada ya kwanza katika mambo ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Utah State na shahada ya uzamili ya utawala wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Tulsa. Amefanya kazi katika sekta ya bidhaa za matibabu, ikiwa ni pamoja na Baxter International kama makamu mwandamizi wa rais na rais wa kampuni wa kanda ya Amerika, na hivi karibuni kabisa kama mjumbe wa bodi ya HemaSource.

Wakati wa wito wake, Mzee Eyre alikuwa akihudumu kama Sabini wa Eneo. Pia amehudumu kama rais wa kigingi, mshauri katika urais wa kigingi, mshiriki wa baraza kuu, askofu, rais wa Wavulana wa kata, na mwalimu wa seminari ya mapema asubuhi.