“Mzee Aaron T. Hall,” Liahona, Mei 2025.
Mzee Aaron T. Hall
Sabini Mkuu mwenye Mamlaka
Mzee Aaron T. Hall anakumbuka wakati yeye na mkewe, Kimberly, waliposimikwa kama viongozi wa misioni katika Misioni ya Texas Houston South. Walimwambia Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kwamba hisia zao zilikuwa kutoka kuzidiwa hadi kuwa na msisimko. Mzee Bednar alielezea haja ya kuwa na shukrani.
“Kile alichotufundisha siku hiyo hakijawahi kutoka mawazoni mwangu kuhusiana na wito wowote tunaopokea, ambao kwa ajili ya huo, ‘Tunashukuru tu,’” alisema. “Unajiuliza ni kwa jinsi gani ulimwenguni Bwana angekuchagua wewe, lakini tunashuhudia kwamba Yeye anafanya hivyo. Na kwa sababu tuko radhi na tunapatikana, Yeye atatufanya tuweze.”
Aaron Tracy Hall alizaliwa mnamo Machi 4, 1971, huko Provo, Utah, mwana wa Alan Eugene Hall na Paula Jeanne Nowak Hall. Alihudumu misioni katika Misioni ya Chile Osorno na baadaye kumwoa Kimberly Wade Hall mnamo Desemba 28, 1993, katika Hekalu la Logan Utah. Wao ni wazazi wa watoto wanne.
Wakati wa wito wake, Mzee Hall alikuwa akihudumu kama Sabini wa Eneo katika Eneo la Utah. Pia amehudumu kama mshauri katika urais wa kigingi, mjumbe wa baraza kuu, katibu mtendaji wa kigingi, askofu, rais wa akidi ya wazee, na rais wa Wavulana katika kata.
Mzee Hall alipata shahada ya kwanza katika mauzo ya kitaaluma kutoka Chuo Kikuu cha Weber State na shahada ya uzamili ya utawala wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Utah. Awali alikuwa mtendaji wa teknolojia na makampuni binafsi ya usawa, hivi karibuni alifanya kazi kama mkurugenzi katika Idara ya Kazi ya Umisionari katika Kanisa.