“Mzee Brian J. Holmes,” Liahona, Mei 2025.
Mzee Brian J. Holmes
Sabini Mkuu mwenye Mamlaka
Mzee Brian J. Holmes alisema yeye na mkewe, Maggie, ni mashahidi wa ahadi ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 84:88 kwamba Yeye “atakwenda mbele ya uso wako.”
“Hicho ndicho alichotutendea maisha yetu yote,” Mzee Holmes alisema. “Tunapogeuza maisha yetu kumgeukia Bwana, Yeye anaweza kufanya mengi kutoka kwenye maisha yetu kuliko tunavyoweza kufanya peke yetu.”
Katika jukumu lake jipya kama Sabini Mkuu mwenye Mamlaka, Mzee Holmes anatarajia atakuwa na fursa za kushuhudia juu ya jukumu kuu la Yesu Kristo katika mpango wa Baba wa Mbinguni.
“Yeye ni Mwokozi na Mkombozi wa watoto wote wa Baba yetu wa Mbinguni,” alisema.
Brian J. Holmes alizaliwa Desemba 5, 1977, jijini Salt Lake, Utah, mmoja wa watoto 12, kwa Michael H. Holmes na Marian R. Holmes. Akiwa kijana mdogo alitumikia misioni yake huko Munich, Germany. Baadaye alimuoa Maggie Wilson katika Hekalu la Salt Lake mnamo Machi 29, 1999. Mzee na Dada Holmes ni wazazi wa watoto sita na walikuwa wakiishi Queen Creek, Arizona, wakati wa wito wake.
Mzee Holmes alipata shahada ya kwanza katika sayansi ya siasa na shahada ya uzamivu ya sheria za mahakama kutoka Chuo Kikuu cha Arizona State. Amefanya kazi kama makamu wa rais wa Holmes Homes huko Arizona, alianzisha kampuni ya Sheria ya Holmes, PLC, na hivi karibuni alifanya kazi kama mshauri mkuu wa Charter One, LLC.
Kabla ya wito wake kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka, Mzee Holmes alikuwa akihudumu kama Sabini wa Eneo katika Eneo la Amerika Kaskazini Kusini Magharibi. Pia amehudumu kama rais wa kigingi, mshiriki wa baraza kuu, na askofu.