2025
Zawadi Kuu za Milele: Upatanisho wa Yesu Kristo, Ufufuko, Urejesho
Mei 2025


13:56

Zawadi Kuu za Milele: Upatanisho wa Yesu Kristo, Ufufuko, Urejesho

Tunapata katika Pasaka katika amani ya Kristo, kuweza kuwa na kuwa sehemu ya—kile ambacho ni cha kudumu na cha shangwe, cha furaha na milele.

Miaka mingi iliyopita, darasa letu la injili la mapema asubuhi lilikuwa la kukariri mistari ya Biblia. Kwa kweli mimi nilivutiwa na vifungu vya maneno vifupi. Hii ilijumuisha Yohana 11:35—aya fupi zaidi katika maandiko, ni maneno mawili tu—“Yesu alilia.”

Kwangu mimi sasa, kwamba Yesu analia kwa huzuni na shangwe inashuhudia juu ya uhalisia wa kimiujiza: Mwana mtakatifu wa Mungu alikuja kimwili duniani na akajifunza kulingana na mwili jinsi gani daima anaweza kuwa nasi na kutubariki.

Tunalipolia kwa huzuni au shangwe, Yesu Kristo anaelewa kikamilifu kabisa. Yeye anaweza kuwa yupo katika nyakati ambazo tunahitaji zaidi zawadi kuu za milele: Upatanisho wa Yesu Kristo, Ufufuko, urejesho.

Yesu akilia.

Mariamu na Martha walilia kwa ajili ya kaka yao Lazaro, ambaye alikuwa amefariki. Kwa huruma, Yesu analia. Anamfufua Lazaro.

Yesu anaiona Yerusalemu siku ya mkesha wa Pasaka. Yeye analia, kwa kushindwa kuwakusanya watu Wake, kama kuku akusanyavyo vifaranga wake. Leo Upatanisho Wake unatupa matumaini tunapohuzunika kwa kile ambacho kingekuwa.

Bwana wa shamba la mizabibu analia anapowaagiza watumishi Wake, ambao ingeweza kujumuisha na sisi kama akina kaka na akina dada watumishi, “Je, ningefanya nini zaidi kwa ajili ya shamba langu la mzabibu?”

Mariamu anasimama akiwa mnyonge kaburini. Yesu kwa upole anamwuliza, “Kwa nini unalia?” Yeye anajua “kulia kunaweza kudumu kwa usiku mmoja, lakini furaha huja asubuhi.” Ufufuko unaleta pambazuko kwa watu wote.

Katika nchi za Kitabu cha Mormoni, umati wa walio waaminifu unainuka kuja Kwake, shangwe ya Yesu imejaa. Yeye analia.

“Na aliwachukua watoto wao wachanga, mmoja mmoja, na kuwabariki, na kuomba kwa Baba juu yao.

“Na baada ya kufanya hivi alilia tena.”

Hii ni Pasaka katika Yesu Kristo: Yeye anajibu matamanio ya mioyo yetu na maswali ya nafsi zetu. Yeye anafuta machozi yetu, isipokuwa machozi ya shangwe yetu.

Machozi yetu yanapotiririka, wakati mwingine tunaomba msamaha, tunaaibika. Lakini kwa kujua kwamba Yesu Kristo huelewa huzuni na shangwe za maisha yetu hilo hutupatia nguvu zaidi ya tulizonazo sisi wenyewe tunapopitia machungu na matamu.

Huko Amerika ya Kusini, baba analia. Mwanga katika maisha yake, binti yake mdogo, amefariki dunia. “Nitatoa chochote ili kumwona tena,” alilia mikononi mwangu. Nami nililia pia.

Mzee Gong kwenye Uwekaji wakfu wa hekalu la Puebla Mexico.

Kwenye uwekaji wakfu Hekalu la Puebla Mexico, machozi ya furaha yalilowesha uso wa dada mmoja mpendwa. Sura yake iliangaza imani na dhabihu. Yeye anasema, “Todos mis hijos están aqui en el templo hoy”—“Watoto wangu wote wako humu hekaluni leo.” Vizazi kukusanyika katika nyumba ya Bwana, inaleta machozi ya shangwe na shukrani.

Katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe, familia na jirani walifanyiana mambo yasiyoweza kusemekana. Machozi ya hasira pole pole yanatoa njia ya tumaini. Sauti yake ikitetemeka, mwanamke mmoja katika kijiji kidogo anasema, “Jirani kabla sijaenda kaburini mwangu, ninataka wewe ujue pale unaweza kuwapata wanafamilia wako wanaokesekana.”

Bibi harusi mwenye kung’ara na bwana harusi mwenye kupendeza wanaunganishwa katika nyumba ya Bwana. Ana umri wa miaka 70, kama mumewe. Bibi harusi mrembo, alikuwa anastahili siku hii. Bibi harusi kwa soni, aliweka vazi lake la harusi liwe hivi, mara liwe vile. Tulimwaga machozi ya shangwe. Ahadi za Mungu zinatimizwa. Maagano Yake huleta baraka.

Wakati akimfundisha nyumbani dada mjane mmoja, kijana Boyd K. Packer alijifunza somo moja muhimu. Kufuatia kutokukubaliana na mume wake, dada huyu alizungumza maneno ya mwisho yaliyomuumiza. Ajali isiyo tarajiwa ilitoa uhai wa mume wake siku ile. “Kwa miaka hamsini,” mjane huyu alilia kwa kwikwi, “Nimeishi jehanamu kwa kujua kwamba maneno ya mwisho aliyosikia kutoka katika midomo yangu yalikuwa machungu, ya chuki.”

Pasaka katika Kristo inatusaidia kurekebisha, kupatanisha, kuweka sawa uhusiano wetu, pande zote mbili za pazia. Yesu anaweza kuponya huzuni, Yeye anaweza kuwezesha msamaha. Yeye anaweza kutuweka huru sisi na wengine kutokana na vitu ambavyo sisi au wengine wamesema au kufanya ambavyo vinginevyo hutuweka utumwani.

Pasaka katika Yesu Kristo hutufanya sisi tuhisi idhinisho la Mungu. Ulimwengu huu unatuambia kwamba sisi ni warefu sana, wafupi sana, wapana sana, wembamba sana, wajanja sana—tusio na akili sana, warembo, au wa kutosha kiroho. Kupitia mabadiliko ya kiroho katika Kristo sisi tunaweza kuepuka ukamilifu wa kulemaza.

Kwa shangwe ya Pasaka, sisi tunaimba, “Mauti ameshindwa; mwanadamu yu huru. Kristo ameleta ushindi.” Ufufuko wa Kristo unatuweka huru kutokana na mauti, kutokana na nyakati za udhaifu na kasoro za kimwili. Upatanisho wa Yesu Kristo pia unaturejesha kiroho. Yeye alitokwa na damu katika kila kinyweleo, akilia machozi ya damu kama ilivyokuwa, ili kutuepusha kutoka dhambini na kutengwa. Yeye anatuunganisha, kikamilifu na kitakatifu, na kila mmoja wetu na Mungu. Katika vitu vyote vizuri, Yesu Kristo anarejesha kwa wingi—siyo tu kile kilichokuwa bali pia kile kinachoweza kuwa.

Maisha na nuru ya Yesu vinashuhudia juu ya upendo wa Mungu kwa watoto Wake wote. Kwa sababu Mungu Baba yetu anawapenda watoto Wake wote katika kila umri na nchi, tunapata mwaliko Wake wa upendo wa kuja kupata amani na shangwe katika Yeye katika desturi nyingi na tamaduni. Mahali popote, wakati wowote, mtu yeyote, tunashiriki utambulisho wa kiungu kama watoto wa Muumbaji yule yule. Katika roho hiyo hiyo, wafuasi wa Uislamu, Uyahudi na Ukristo wanashiriki urithi wa kidini katika Baba Ibrahimu na muunganiko wa kiagano kupitia matukio huko Misri ya kale.

Baba Ibrahimu alikuja Misri na alibarikiwa.

Yusufu, aliuzwa utumwani huko Misri, alijua ndoto ya Farao ilimaanisha miaka saba ya neema ikifuatiwa na miaka saba ya baa la njaa. Yusufu aliokoa familia yake na watu wake. Yusufu alilia alipoona mpango mkubwa wa Mungu, ambamo mambo yote yatafanyika kwa pamoja kwa faida ya wale wanaoshika maagano yao.

Musa, alilelewa huko Misri katika kaya ya Farao, alipokea na baadaye kurejesha funguo za kuwakusanya watoto wa Mungu.

Yusufu, Mariamu, na Yesu wakitorokea Misri.

Wakitimiza unabii, Yusufu, Mariamu na mtoto mchanga Kristo walikimbilia huko Misri. Huko Kairo, Muislamu wa dhati aminiye kwa unyenyekevu anasema: “Kuran inafundisha kwamba Yusufu, Mariamu na mtoto Yesu walipata usalama na mahali patakatifu katika nchi yangu. Katika nchi yangu, Yesu kama mtoto mchanga alikula chakula chetu, alitembea hatua Zake za kwanza, alisema maneno Yake ya kwanza. Hapa katika nchi yangu, tunaamini miti iliinama chini ili kumpa Yeye na familia Yake matunda. Kuwepo Kwake katika nchi yangu kulibariki watu na nchi.”

Mpango wa Mungu juu ya maadili na haki ya kujiamulia duniani vinaturuhusu kujifunza kwa uzoefu wetu sisi wenyewe. Baadhi ya masomo makuu ya maisha yanakuja kutokana na mambo ambayo tusingeweza kuchagua. Katika upendo, Yesu Kristo alijishusha chini na kupanda juu ya vitu vyote. Yeye anafurahia katika uwezo wetu wa kiungu wa ubunifu na furaha, ukarimu pasipo matumaini ya thawabu, imani katika toba na msamaha. Na analia kwa huzuni kwa wingi wa mateso yetu ya kibinadamu, ukatili, ukosefu wa haki—mara nyingi vikiletwa na chaguzi za kibinadamu—kama ilivyo kwa mbingu na Mungu wa mbinguni pamoja nao.

Kila majira ya kuchipua ya Pasaka yanashuhudia kwamba mfuatano na muunganiko wa kiroho vyote ni sehemu ya mpangilio wa kiungu wa upatanisho, ufufuko na urejesho kupitia Yesu Kristo. Muunganiko huu mtakatifu unakuja siyo kama ajali au kwa bahati tu. Jumapili ya Matawi, Wiki Takatifu na Pasaka husherehekea Upatanisho na Ufufuko wa Yesu Kristo. Kama leo, kila siku ya Aprili 6 tunakumbuka kuanzishwa na kuundwa kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Urejesho huu ndio sababu tunakusanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi wa Aprili katika mkutano mkuu.

Urejesho pia ulikuja pale Yesu Kristo aliyefufuka, Musa, Elia na Eliya, waliporejesha funguo za ukuhani na mamlaka kwenye Hekalu jipya na lililowekwa wakfu la Kitland siku ya Jumapili ya Pasaka, 1836. Katika mazingira yale siku ile kwa urejesho wa Kanisa la Yesu Kristo yalikuja mamlaka ya Mungu na baraka ya kuwakusanya watoto Wake, kuwaandaa watoto Wake kurudi Kwake na kuziunganisha familia milele. Urejesho siku ile ulitimiza unabii kwa kutokea katika siku ya Pasaka na Kumbukizi ya kukombolewa kwa wana wa Israeli kutoka utumwani Misri.

Mzee Gong katika Hekalu la Kirtland

Ikijumuisha Hekalu la Kirtland, hivi karibuni nilitembelea maeneo matakatifu huko Ohio mahali ambapo Nabii Joseph na wengine walimwona katika ono Mungu Baba yetu na Mwana Wake Yesu Kristo. Nabii Joseph aliona jinsi mbinguni kulivyo. Huko mbinguni, Baba wa Mbinguni, kupitia Yesu Kristo, “anaokoa kazi zote za mikono Yake” katika ufalme wa utukufu. Tofauti pekee ni kwa wale ambao kwa makusudi “wanamkana Mwana baada ya kuwa Baba amemfunua.”

Huduma Yake ya duniani ilipoanza, Yesu alitamka misheni Yake ya kutubariki kila mmoja kwa vyote tulivyo tayari kupokea—katika kila wakati, kila nchi, kila hali. Baada ya kufunga kwa siku 40, Yesu alienda katika sinagogi na kusoma “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema, amenituma kuponya waliovunjika moyo, kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa.”

Maskini, waliovunjika moyo, wafungwa, vipofu, waliojeruhiwa—hiyo ni kila mmoja wetu.

Kitabu cha Isaya kinaendeleza ahadi ya Kimasiya ya tumaini, ukombozi, uhakika: “Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, … wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito.”

Hivyo, sisi tunalia, “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki.”

Kila majira ya Pasaka tunasherehekea, kama ishara, zawadi kuu za milele kupitia Yesu Kristo: Upatanisho Wake, Ufufuko Wake halisi (na ahadi ya ufufuko wetu halisi), Urejesho wa Kanisa Lake la siku za mwisho lenye funguo za ukuhani na mamlaka ya kuwabariki watoto wote wa Mungu. Tunashangilia katika mavazi ya wokovu na vazi la haki. Tunapiga kelele, “Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo!“

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Na kila mmoja wetu apate katika Yesu Kristo upatanisho, ufufuko na urejesho—amani, kuwa, na kuwa wa sehemu ya—kile ambacho kinadumu kweli na chenye shangwe, furaha na kisicho na mwisho, ninaomba katika jina Lake takatifu, Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Alma 7:11–12. Kumbuka pia ahadi za kimaagano katika ibada ya sakramenti: Tunajichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, “daima kumkumbuka na kushika amri zake … ; ili daima Roho wake apate kuwa pamoja [nasi]” (Mafundisho na Maagano 20:77).

  2. Ona Yohana 11:33–35, 39-44.

  3. Ona Luka 7:41–44; ona pia Mathayo 11:37–21; Marko 1:34.

  4. Yakobo 5:41.

  5. Yohana 8:15.

  6. Zaburi 30:5

  7. 3 Nefi 5:21–22.

  8. Ona Zaburi 107:9; Yeremia 33:3.

  9. Ona Isaya 25:8.

  10. Ona Alma 26:12.

  11. Boyd K. Packer, “The Saints Securely Dwell,” Ensign, Jan. 1973.

  12. “Kafufuka!,” Nyimbo za Dini, no. 111, echoes the glad tidings of 2 Nephi 9:10—Jesus Christ “prepareth a way for our escape from the grasp of this awful monster; yea, that monster, death and hell, … the death of the body, and also the death of the spirit.”

  13. Ona Mwanzo 37-47. Yusufu kumleta baba yake, Yakobo, na familia yake huko Misri kunawakilisha kuungana tena kwa upendo kwa mwana na baba waliotenganishwa kwa muda mrefu. Inakuwa pia njia ambayo kwayo familia ya Yakobo na kizazi cha agano, ambao watajumuishwa Lehi na familia yake watahifadhiwa. Ona 1 Nefi 5:14–15; 6:2.

  14. Ona Mwanzo 45:1–8.

  15. Ona Warumi 8:28; Mafundisho na Maagano 90:24; 98:3.

  16. Ona Mafundisho na Maagano 110:11; Ona pia Marko 9:2–10; Luka 9: 28–36.

  17. Ona Mathayo 2:13–15.

  18. Ona Mafundisho na Maagano 88:6; 122:8.

  19. Ona Musa 7:28.

  20. Tunazungumza juu ya majira ya kuchipua ya Pasaka, tukitambua kwamba Pasaka inaweza kuja mwezi Machi au Aprili na kwamba majira ya kuchipua katika dunia ya kaskazini kwa kawaida inakuja mwezi Machi au Aprili. Bila kujali juu ya tarehe mahususi ya Pasaka, majira ya Pasaka yanatukumbusha juu ya zawadi hizi kuu za milele kupitia Yesu Kristo.

  21. Ona Mafundisho na Maagano 21:3; 115:4.

  22. The sacred anniversaries that occur each Easter season sometimes exactly coincide. For example, Easter and general conference occur on the same Sunday in 2026 and 2029. Palm Sunday and general conference occur on the same Sunday in 2031 and 2034. Passover occurs near to Easter and during general conference in 2026 and 2029. Bila kujali kama ni ndio au hapana kwa kumbukubu hizi kuwa sawa, tunaelewa ukaribu wao wa kuunganika sio kwa bahatu tu au ajali; ni mtakatifu na ni wa kiishara.

  23. Ona Mafundisho na Maagano 110.

  24. Mafundisho na Maagano 76:43; ona pia mstari wa 42.

  25. Rais Dallin H. Oaks anafundisha: “Madhumuni ya Kanisa hili la urejesho ni kuwaandaa watoto wa Mungu kwa ajili ya wokovu katika utukufu wa selestia na, kwa kipekee zaidi, kwa ajili ya kuinuliwa katika kiwango cha juu zaidi” (“Falme za Utukufu,” Liahona, Nov. 2023, 27).

  26. Mafundisho na Maagano 76:43.

  27. Luka 4:18; ona pia Isaya 61:1.

  28. Isaya 61:3.

  29. Isaya 61:10.

  30. Mafundisho na Maagano 109:79.

  31. Yohana 3:16.