“Mzee Pedro X. Larreal,” Liahona, Mei 2025.
Mzee Pedro X. Larreal
Sabini Mkuu mwenye Mamlaka
Katika mwezi wa nne wa Mzee Pedro X. Larreal kama mmisionari, Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alitembelea Misioni ya Venezuela Caracas.
Mzee Larreal alikumbuka, “Alitoa mwaliko wa kupendeza kwetu kuhusu kuweka wakfu: ‘Kama utafokasi kwa asilimia 100, ninakuahidi familia yako ya baadaye itapokea baraka.’”
Baadaye, Mzee Larreal aliandika barua ya kuachana na rafiki yake wa kike huko nyumbani. “Nilihitaji kuweka kila kitu kwenye madhabahu kwa sababu nilihitaji kufokasi zaidi.”
Akitazama nyuma, anatambua baraka nyingi—elimu yenye manufaa, ajira yenye mafanikio—ikichipuka kutoka katika kutumaini katika ahadi hiyo ya kitume.
“Tunapofuata maelekezo ya nabii, mwonaji, na mfunuzi, tutapata baraka katika maisha yetu,” alisema. “Ninaahidi”
Pedro Xavier Larreal Noguera alizaliwa Julai 6, 1976, huko Valencia, Venezuela, kwa Duilio Antonio Larreal Romero na Haydee Maria Noguera De Larreal. Alimuoa Saria Alvarez Campos katika Hekalu la Caracas Venezuela mnamo Agosti 25, 2001. Wao ni wazazi wa watoto watatu.
Mzee Larreal alipata shahada ya usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Simón Rodríguez, shahada ya uzamili ya sayansi katika elimu kutoka Chuo Kikuu cha Santa Maria, na shahada ya uzamili ya utawala wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Brigham Young. Alifanya kazi kama mratibu wa Seminari na Vyuo vya Dini na alifanya kazi kwa ajili ya Nature’s Sunshine Products Inc. kama meneja mkuu na mkurugenzi wa Eneo la Mexico, Amerika ya Kati, na Jamhuri ya Dominika.
Kabla ya kuitwa kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka, Mzee Larreal alikuwa akihudumu kama rais wa Misioni ya Texas McAllen. Amehudumu kama Sabini wa Eneo katika maeneo mawili, rais wa kigingi, mshauri katika urais wa kigingi, mshiriki wa baraza kuu, katibu mtendaji wa kigingi, na askofu.