“Mzee John D. Amos,” Liahona, Mei 2025.
Miito Mipya
Mzee John D. Amos
Sabini Mkuu mwenye Mamlaka
Mnamo mwaka 2020, Mzee John D. Amos alipokea wito wenye kubadilisha maisha kuwa rais wa Misioni ya Baton Rouge Louisiana. Mambo mengi katika maisha yake yalihitaji mabadiliko kwa sababu ya wito huu, lakini Mzee na Dada Amos kwa neema walikubali kazi hiyo kwa imani.
“Uamuzi na msimamo tayari vilifanywa muda mrefu uliopita,” alisema Mzee Amosi. “Bwana anapoita, tunajibu tu.”
John D. Amos alizaliwa Novemba 2, 1961, huko Lafayette, Louisiana, kwa John N. Amos Sr. na Dorothy Victorian Amos. Alikutana na aliyetarajia kuwa mkewe, Michelle Evette Wright, kupitia madarasa waliyohudhuria pamoja chuoni, wakichukua kozi ya uhandisi wa umeme.
Michelle, ambaye tayari alikuwa muumini wa Kanisa, alimwalika John kwenye dansi ya kanisa kwenye miadi yao ya kwanza. Baada ya hapo, alianza kujifunza zaidi kuhusu Kanisa na jukumu kuu la Mwokozi katika injili ya urejesho.
“Kila kitu ni kuhusu Yesu Kristo,” alisema. “Yeye Ndiye kiini cha shangwe yote.”
Mzee Amos na Michelle walioana Juni 9, 1990, katika Hekalu la Atlanta Georgia. Wana watoto watatu na wajukuu sita.
Mzee Amos amepata shahada katika uhandisi wa umeme na nyuklia. Wakati wa kazi yake, alihudumu katika Jeshi la Wanamaji la Marekani, alifanya kazi katika Siemens Energy Inc, na alifundisha katika Chuo Kikuu cha Florida Central.
Miito yake iliyopita ya Kanisa ni pamoja na Sabini wa Eneo (Eneo la Kaskazini kusini Mashariki), rais wa misioni, mshauri katika urais wa kigingi, askofu, mshauri wa uaskofu, rais wa Shule ya Jumapili katika kata, katibu mtendaji wa kata, kiongozi wa kundi la makuhani wakuu, na kiongozi wa watoto wadogo zaidi.