2025
Kuthamini Maisha
Mei 2025


14:10

Kuthamini Maisha

Uhai ni sehemu ya thamani sana ya mpango mkamilifu wa Baba, na kwa amri Yake tunathamini na kuhifadhi uhai.

Mwokozi wetu, Yesu Kristo, alitufundisha, “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”

Askofu huko Utah alishiriki nami hivi karibuni kuhusu upendo mwingi katika kata yake kwa ajili ya binti na familia yake. Kupitia mtiririko wa matukio mazuri, wazazi walinuia kurejea kwa Mwokozi na Kanisa Lake. Wakati walipokuwa mbali na Kanisa, binti yao kijana alijihusisha kwenye mahusiano na kijana wa kiume. Akirejea, binti huyu wa thamani alihisi upendo mwingi kutoka kwa Baba wa Mbinguni wakati wa mkutano wa ushuhuda wa Wasichana. Aliazimia kuishi amri kikamilifu zaidi. Aliandika, “Nilianza mchakato wa toba pamoja na askofu wangu.”

Punde baadaye, alikuwa mgonjwa. Kwa maneno yake: “Kipimo kilionyesha … nina mimba. Nilianza … kulia. … Baba yangu alinikumbatia katika mikono yake na kunihakikishia kwamba kila kitu [kingekuwa] SAWA. … Yule kijana wa kiume … aliniambia nitoe mimba. … Nilikataa.”

Kuwatunza wale wenye mahitaji.

Binti aliendelea: “Nimepokea upendo mwingi na msaada kutoka katika kata ya familia yangu. Hili ni jambo la kutia moyo sana. Askofu [wangu] na rais wa Wasichana wamefanya zaidi kwa kuonyesha upendo wao na msaada. … Nimeuona mkono wa Bwana … ukiniongoza mimi na familia yangu. … Kata kama ya kwangu ni familia ambayo kila mmoja anaihitaji, hasa binti katika hali yangu.”

Yeye na familia yake na kata ya familia yake kwa upendo walimkaribisha mtoto wake wa kiume mwezi Februari iliyopita.

Bwana Yesu Kristo.

Rais Russell M. Nelson alisema, “Sifa bainifu ya Kanisa la kweli na lililo hai la Bwana daima itakuwa ni jitihada zenye utaratibu … zilizoelekezwa kuwahudumia watoto wa Mungu mmoja mmoja na … [kuhudumia kwa wema wa upendo] kwa yule mmoja, kama Yeye alivyofanya.”

Kusaidia Chaguzi Njema

Pale mwanamke asiye na mwenza anapogundua kwamba anatarajia mtoto ambaye hakupanga kumpata, maswala ya afya, maumivu ya roho, aibu, woga wa kifedha, maswali kuhusu elimu, wasiwasi wa ndoa na huzuni ya ndoto zilizoharibika vinaweza, katika hali ya maumivu na majuto, kupelekea mwanamke huyo kuchukua hatua zitakazopelekea maumivu makali na huzuni.

Kwa yeyote anayesikiliza ambaye amepitia maumivu makali na majuto kwa au kushiriki katika kutoa mimba, tafadhali kumbuka: Ingawa hatuwezi kubadili yaliyopita, Mungu anaweza kuponya hayo yaliyopita. Msamaha unaweza kuja kupitia miujiza ya neema Yake ya upatanisho pale unapomgeukia Yeye kwa moyo mnyenyekevu na wa toba.

Mara nyingi maneno mawili huambatanishwa kwenye utakatifu wa uhai wa duniani: uhai na uchaguzi. Uhai ni sehemu ya thamani sana ya mpango mkamilifu wa Baba, na kwa amri Yake tunathamini na tunahifadhi uhai; na tunachagua mwendelezo wa uhai wakati wa ujauzito. Pia tunathamini zawadi ya chaguo la uhuru wa kujiamulia kimaadili—kusaidia kuimarisha chaguzi za haki zilizoidhinishwa na Mungu ambazo huleta furaha ya milele.

Pale mwanamke na mwanamume wanapokuwa katika wakati dhaifu kama huu, wakikabiliana na chaguzi muhimu, maneno yetu, mikono yetu, mioyo yetu—kiroho, kihisia na kifedha—tunaweza kuwabariki kuhisi upendo wa Mwokozi na kama Rais Henry B. Eyring alivyosema, kutoa marekebisho kwa macho yao ya kiroho kutoka “kwenye kile wanachodhani wanakiona” hadi “kwenye kile ambacho bado hawakioni.”

Mafundisho ya Maisha ya Duniani

Rais Dallin H. Oaks alisema: “Mtazamo wetu kuhusu utoaji mimba haujajengwa kwenye maarifa yaliyofunuliwa ya ni lini uhai wa duniani huanza. … Umejikita kwenye maarifa yetu kwamba … wote wa watoto wa kiroho wa Mungu lazima waje kwenye ulimwengu huu kwa lengo tukufu, na utambulisho wa mtu huyo ulianza kitambo hata kabla ya kuwa mimba na utaendelea kwa milele zote zijazo.”

Neno la Bwana kuwahusu ambao hawajazaliwa, likipewa sauti kupitia Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, halijabadilika kamwe na hutoa mwangwi kwa maneno ya manabii kwa vizazi, likitoa uwazi wa kiungu kwa kile ambacho Bwana ametuomba sisi.

“Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huamini katika utakatifu wa uhai wa binadamu. Kwa hivyo, Kanisa linapinga utoaji wa mimba kwa hiari kwa sababu binafsi au za kijamii, na linawashauri waumini wake kutokukubali, kutotekeleza, kutohimiza, kutolipia au kupanga utoaji wa mimba wa aina hiyo.

“[Bwana] anaruhusu dharura kadhaa yamkini… pale:

  • Mimba itokanayo na ubakaji au kujamiiana kwa maharimu, au

  • Daktari mtaalamu amegundua kwamba maisha au afya ya mama iko katika hatari kubwa, au

  • Daktari mtaalamu anapoamua kwamba kijusi kina kasoro kubwa ambazo hazitaruhusu mtoto kuishi baada ya kuzaliwa.”

Urais wa Kwanza unaendelea: “Utoaji mimba ni jambo zito sana. [Hata katika hali hizi nadra] linapaswa kufikiriwa tu baada ya wahusika kuwa wamepokea uthibitisho kupitia sala” na kushauriana wao kwa wao.

Miaka thelathini iliyopita, manabii wa Mungu walitoa tangazo kwa ulimwengu. Hujumuisha maneno haya:

“Tunatangaza … kwamba Mungu ameamuru kwamba nguvu takatifu za kuzaa ni lazima zitumike tu, kati ya mwanamume na mwanamke, ambao wameoana kihalali kama mume na mke.

“Tunatangaza njia ambayo maisha ya dunia yanaumbwa imechaguliwa kitakatifu. Tunathibitisha utakatifu wa uhai na umuhimu wake katika mpango wa milele wa Mungu.”

Kutunza na kulinda maisha ambayo hayajazaliwa siyo jambo la kisiasa. Ni sheria ya maadili iliyothibitishwa na Bwana kupitia manabii Wake.

Kuzungumza kwa Uwazi Zaidi

Kauli ya Rais J. Reuben Clark Mdogo ambaye alitumikia katika Urais wa Kwanza, kwa uzuri huelezea vijana wetu leo: “Vijana wa Kanisa wana njaa ya vitu vya Roho; wana hamu ya kujifunza injili, na wanaitaka moja kwa moja, bila kuzimuliwa.” Wanataka kujua kuhusu … imani zetu; wanataka kupokea ushuhuda wa ukweli huu. Wao ni … wadadisi, watafutaji wa ukweli.” Acha tuzungumze mara kwa mara kwa imani na huruma kwa vijana wetu katika nyumba zetu, na mmoja na mwingine, katika Muungano wetu wa Usaidizi na mikutano ya akidi za wazee kuhusu sheria ya usafi wa kimwili ya Bwana, utakatifu wa uhai, na matunzo kwa ambao hawajazaliwa na mama zao.

Dada mpendwa aliniandikia uzoefu alioupata miongo kadhaa iliyopita: “Kama binti wa miaka 17 … , nilijipata nikiwa mjauzito bila ya msaada wowote kutoka kwa mpenzi wangu. Nilihisi kuaibika na mpweke [lakini] sikufikiria [utoaji mimba]. … Nilikuwa na familia yangu pendwa na askofu wangu, ambaye nilikutana naye mara kwa mara kwa ajili ya mwongozo. … Nilimgeukia Mungu. Nilisoma maandiko … na kusali [na] kupata nguvu kupitia Mwokozi wangu na mchakato wa toba. … Nilipokea jibu [la sala zangu] ambalo nisingeweza kulikana. … Lilikuwa la kuvunja moyo, lakini nilijua ningemtoa binti yangu kwa ajili ya kuasiliwa. … Nilisali kwa ajili ya ujasiri [na] kuhisi upendo wa Mwokozi kwa dhahiri kupitia toba, ninajua kwamba Mungu … hujibu sala na kutuimarisha.”

Wenza wenye upendo walimuasili binti mtoto wa thamani na walimfunza injili. Sasa binti huyo ameolewa na ana familia yake nzuri.

Wakati mwingine, mashaka magumu sana na yaumizayo sana yanaweza kuambatana na ulinzi wa uhai.

Hivi karibuni wenza vijana ambao Kathy pamoja nami tunawapenda waliniandikia kuhusu mtoto mchanga wanayemtarajia.

Baba aliandika: “[Mke wangu alipokuwa] na ujauzito wa wiki 10 tuligundua kwamba mtoto wetu wa muujiza alikuwa na hali ya vinasaba ya traisomi 21, hali ijulikanayo kama shida kwenye ubongo. Tulihisi shinikizo … kutoka kwenye kitengo cha afya la kutoa ujauzito. Wiki chache baadaye tuligundua … mtoto wetu ambaye hajazaliwa … angehitaji upasuaji wa moyo mara kadhaa katika mwaka wake wa kwanza wa uhai. Kupitia mchakato huu kadiri tulivyosali kwa dhati kwa ajili ya msaada wa kiungu, … tumehisi Roho akitupatia faraja. Tulipokea ufunuo na uelewa kwamba binti yetu ni mtoto makini wa Baba wa Mbinguni na ana hamu kubwa ya kuwa kwenye familia yetu na kuja duniani.”

Mama wa mtoto mchanga aliandika: “Tulishtushwa, kukanganyikiwa na kwa kweli, kukatishwa tamaa kwa taarifa hiyo. … Nilipokuwa na mimba ya miezi 14, tuligundua kwamba mtoto wetu alikuwa na madhaifu kadhaa ya moyo ya kuzaliwa nayo, ambayo yangepelekea kifo. Tulionana na madaktari wengi na wataalamu kutokea kipindi cha wiki 10–18. … Katika kila moja ya miadi yetu, tuliulizwa kama tunahitaji kuendelea kuutunza ujauzito au kuuharibu. … Mwokozi alitibu moyo wangu na kunipa hisia ya amani na furaha kuhusu mtoto wetu wa kike. … [Baba wa Mbinguni] amenionyesha mara kwa mara na tena kwamba Yeye ana mpango mkamilifu kwa ajili yangu [na] ninamtumaini.”

kwa shangwe walimkaribisha mtoto wao mchanga wiki moja iliyopita siku kama ya leo. Binti ni wao na wao ni wazazi wake daima.

Imani isiyo na shaka na ujasiri mkuu ni alama mahususi za wanafunzi wa Yesu Kristo.

Mfano Mkuu wa Imani

Kwa miaka mingi, nimepata fursa ya kukutana na wanaume na wanawake ambao kwa unyenyekevu wametafuta kurejea kwenye njia ya agano na kwenye baraka zao za ukuhani na hekalu miaka mingi baada ya kupoteza uumini wao.

Katika tukio moja, nilitakiwa kumhoji mwanaume kwa niaba ya Urais wa Kwanza kwa ajili ya urejesho wa ukuhani na baraka za hekaluni.

Baada ya ndoa yake katika hekalu takatifu, na baada ya kupata watoto wazuri watatu, mwanaume hakuwa mwaminifu kwa mke wake na maagano yake matakatifu. Mwanamke mmoja alipata ujauzito na kutaka kuutoa.

Mke wa mume yule kitakatifu alimsihi yule mwanamke kumzaa mtoto na kumuahidi kwamba atamlea mtoto pale atakapozaliwa, pamoja na watoto wake mwenyewe.

Mwanamke yule alikubali kutotoa ujauzito ule.

Sasa imekuwa miaka 10. Dada mnyenyekevu akiwa amekaa mbele yangu alimpenda mtoto kama wake na kuniambia juhudi za mume wake za kurekebisha na kumpenda na kumjali yeye na familia. Baba alilia pale mke alipokuwa akiongea.

Ni kwa jinsi gani mwanamke huyu mwema wa Mungu alimchukulia mtoto kama wa kwake ambaye angekuwa ukumbusho wa kila siku wa ukosaji uaminifu wa mumewe? Kivipi? Kwa sababu alipata nguvu kupitia Yesu kristo na aliamini kwenye utakatifu wa uhai, utukufu wa uhai. Alijua mtoto aliyekuwa hajazaliwa alikuwa mtoto wa Mungu, bila hatia na msafi.

Mkusanyiko wa picha za mtoto.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, kupungua kwa upendo kwa watoto ambao hawajazaliwa ni jambo kubwa ulimwenguni kote. Mungu anathamini uhai. Ni kazi Yake na utukufu kuleta kutokufa na uzima wa milele wa wanadamu. Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tunathamini uhai. “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.” Na tushiriki upendo wetu hata kwa wingi zaidi na wale wanaotuhitaji kweli kweli. Ninatoa upendo wangu kwenu na upendo wa Baba yetu wa Mbinguni kwa watoto Wake wajao duniani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Yohana 13:35; ona pia Mathayo 22:36–40.

  2. Majibu binafsi, Feb. 6, 2025; yametumika kwa ruhusa.

  3. Majibu binafsi, Feb. 6, 2025; yametumika kwa ruhusa.

  4. Russell M. Nelson, “Kuhudumu kwa Nguvu na Mamlaka ya Mungu,” Liahona, Mei 2018, 69.

  5. Mfano wa mwanamke mwema huko Ufaransa; ona Neil L. Andersen, Zawadi Takatifu ya Msamaha (2019), 154–56.

  6. Ona Neil L. Andersen, Zawadi Takatifu ya Msamaha,, 219; ona pia Neil L. Andersen, Yesu Ndiye Kristo (2023), 5.

  7. Ona kauli rasmi kuhusu kutoa mimba: “Abortion,” newsroom.ChurchofJesusChrist.org. Kitabu cha Maelezo ya Jumla kinasema, “Mtu anaweza kutubu na kusamehewa kwa dhambi ya kutoa mimba” (Kitabu cha Maelekezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho, 38.6.1, Gospel Library). Rais Ezra Taft Benson alisema, “Huzuni ya kimungu ni karama ya Roho. Ni utambuzi wa kina kwamba matend yetu yamemhudhi Baba yetu na Mungu wetu. Ni ufahamu dhahiri na wa [kina] kwamba tabia yetu ilimfanya Mwokozi, Yeye ambaye hakuwa na dhambi, hata mkuu wa wote, kuvumilia masumbuko makali na mateso. Dhambi zetu zilimfanya atokwe na damu katika kila kinyweleo. Masumbuko haya halisi sana kabisa ya kiakili na kiroho ni kile maandiko yanarejelea kama kuwa ‘mioyo iliyovunjika na roho zilizopondeka’ [ona Mafundisho na Maagano 20:37]. Roho kama hiyo ndiyo sharti kamili kwa ajili ya toba ya kweli” (Teachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson [2014], 83; ona pia 2 Wakorintho 7:10; 3 Nefi 9:20; 18:32).

  8. “Bwana akamwambia Henoko: Tazama ndugu zako hawa; wao ni kazi ya ustadi wa mikono yangu wenyewe, nami niliwapa maarifa yao, katika siku ile niliyowaumba; na katika Bustani ya Edeni, nikampa mtu haki ya kujiamulia;

    “Na kwa ndugu zako Mimi niliwaambia, na pia nikawapa amri, kwamba yawapasa kupendana, na kwamba yawapasa kunichagua Mimi, Baba yao” (Musa 7:32–33).

  9. Henry B. Eyring, To Draw Closer to God (1997), 143.

  10. Dallin H. Oaks, “The Great Plan of Happiness,” Ensign, Nov. 1993, 74. Rais Nelson amesema: Si swali la lini ‘uhai wenye manufaa’ huanza au lini roho ‘huhuisha’ mwili. Katika sayansi ya baiolojia, inajulikana kwamba uhai huanza pale seli mbili zinapoungana kuwa seli moja, na kutengeneza kromosomu ishirini na tatu kutoka kwa wote baba na mama. … Mwanzo wa uhai sio wa suala la kubishana, lakini ukweli wa kisayansi” (“Reverence for Life,” Ensign, May 1985, 13).

  11. Rais John Taylor alisema mnamo 1879, “Sisi lazima [tutetee] dhidi ya utoaji mimba, uuaji wa watoto wachanga na desturi zingine za kuchukiza … iwe katika utungaji sheria bungeni, maamuzi ya mahakamani au mamlaka yoyote nyingine ya ustaarabu” (“Discourse,” Deseret News, Dec. 31, 1879, 755; spelling modernized).

  12. Ona kauli rasmi kuhusu utoaji mimba: “Abortion,” newsroom.ChurchofJesusChrist.org.

  13. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Gospel Library.

  14. J. Reuben Clark, The Charted Course of the Church in Education, rev. ed. (1994; address to Church Educational System religious educators, Aug. 8, 1938), 3, Gospel Library.

  15. Ona Mada na Maswali, “Abortion,” Gospel Library.

  16. Majibu binafsi, Feb. 13, 2025; yametumika kwa ruhusa.

  17. Mfano mwingine wa baraka ya kuasili ni hadithi ya Sherilyn Stinson na bintiye, Allison, pamoja na mama wa kumzaa wa Allison, Jill Morgenses (ona Mary Ricahrds “Navigating the Journey of Adoption Reunification,” Church News, Nov. 18, 2024, thechurchnews.com.

  18. Kwa msaada wa Bwana na mikono iliyonyooshwa, wengi wanabarikiwa kupata njia yao. Ona Amanda Becker, “Kupata Tumaini kama Mama Mtarajiwa,” Liahona, July 2022 (kidijitali pekee); “The Adoption Decision,” New Era, Mar. 2006, 28–33.

  19. Majibu binafsi, Feb. 17, 2025; yametumika kwa ruhusa.

  20. Uzoefu binafsi; ona Neil L. Andersen, Zawadi Takatifu ya Msamaha, 246–47

  21. Ona Musa 1:39.

  22. Yohana 13:35; ona pia Mathayo 22:36–40.

  23. Nyenzo zingine za msaada: Mada za Injili: Mada na Maswali, “Unwed Pregnancy,” Gospel Library; “Single Expectant Parents,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 38.6.19; Counseling Resources, “Single Expectant Parents,” Gospel Library.