2025
Mzee Eduardo F. Ortega
Mei 2025


“Mzee Eduardo F. Ortega,” Liahona, Mei 2025.

Mzee Eduardo F. Ortega

Sabini Mkuu mwenye Mamlaka

Kwa miaka mingi ya huduma ya Kanisa, Mzee Eduardo F. Ortega amejifunza somo la thamani. Katika wito wowote, iwe kama askofu au kama kaka mhudumiaji, tukijua kwamba tunamwakilisha Bwana, hilo hufanya wito huo kuwa rahisi.

“Tukifikiria jinsi ambavyo Yeye angefanya, ni rahisi zaidi,” alisema, akinukuu Yakobo 5:71–72 katika Kitabu cha Mormoni. “Nimehisi Bwana akihudumu pembeni yangu mara nyingi katika miito mingi kwa sababu ni shamba Lake la mizabibu, sio letu.”

Eduardo Franciso Ortega alizaliwa huko Godoy Cruz, Mendoza, Ajentina, mnamo Julai 10, 1977, kwa Fernando Daniel Ortega na Irma Elvira Endstorfer. Alimuoa Gabriela Alejandra Cappi Franzia katika Hekalu la Montevideo Uruguay mnamo Septemba 13, 2002. Wao ni wazazi wa watoto watano na walikuwa wakiishi Jiji la Mexico, nchini Mexico, wakati wa wito wake.

Mzee Ortega alipata shahada ya kwanza katika usanifu wa majengo na kusimamia ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha John F. Kennedy, Ajentina, mwaka 2008 na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Belgrano mnamo 2016. Mwaka 2017 alipokea diploma katika uongozi kutoka Shule ya Biashara ya Harvard. Alifanya kazi kama meneja wa mradi wa ujenzi, kwanza kwa Kampuni ya SBA na kisha kwa tawi la Ajentina la Village Roadshow Entertainment Group. Alikuwa mkurugenzi wa mali isiyohamishika wa Kampuni ya American Express mwaka 2014, mwanachama wa bodi ya Miradi ya Arch Royale Ltd. mwaka 2023, na mwanachama wa bodi ya CorNet Global mwaka 2024.

Wakati wa wito wake, Mzee Ortega alikuwa akihudumu kama Sabini wa Eneo. Pia amehudumu kama mshauri katika urais wa kigingi, askofu, mshauri katika uaskofu, rais wa akidi ya wazee, kiongozi wa kikundi cha makuhani wakuu, na mmisionari katika Misioni ya Colombia Cali.