2025
Mzee Kevin G. Brown
Mei 2025


“Mzee Kevin G. Brown,” Liahona, Mei 2025.

Mzee Kevin G. Brown

Sabini Mkuu mwenye Mamlaka

Wakati Kevin Brown alipokuwa na umri wa miaka 12, dada mmisionari alimpa changamoto ya kusoma Kitabu cha Mormoni. Kwa hiyo, kila asubuhi angesali, kusoma, na kusali tena. Kwa kila sala, alimuuliza Baba wa Mbinguni kama Kitabu cha Mormoni kilikuwa cha kweli.

Anakumbuka kwamba asubuhi moja wakati akisali, “hakuhitaji hata kuuliza swali. Jibu la Bwana lilikuja kwa njia ya kina sana.” Alihisi Bwana akimwambia: “Ninakujua, na ninakupenda. Wewe ni Mwanangu.”

Mara moja, Roho Mtakatifu alimthibitshia: “Huu ni ukweli wa Mungu. Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Joseph Smith ni nabii.” Uzoefu huu ulibadilisha maisha yake.

Mzee Brown anasifu ushawishi wa dada yule mmisionari na wengine kwa ajili ya mahali alipo sasa. Tangu akiwa na umri mdogo, alishawishiwa na waumini wa Kanisa ambao walimsaidia—kutoka kwa rais wake wa wilaya hadi walimu wa Watoto, kutoka wamisionari vijana hadi wamisionari waandamizi na hasa mke wake, Nadine, ambaye amekuwa na matokeo makubwa zaidi ukiachilia mbali Bwana.

Kevin G. Brown alizaliwa Mei 18, 1976, huko Manchester, Jamaica, kwa Desmond Holness na Patsy Williams Brissett. Alimuoa Nadine Lezanne Carter mnamo 1999. Wana watoto watano.

Mzee Brown alipokea shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia, Jamaica, mwaka 2008. Alipokea shahada ya uzamili katika utawala bora na sera ya umma kutoka Chuo Kikuu cha West Indies mwaka 2012. Tangu mwaka 2001 amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya Seminari na Vyuo vya Dini vya Kanisa.

Wakati wa wito wake, Mzee Brown alikuwa akihudumu kama Sabini wa Eneo katika Eneo la Utah.