“Mzee Ronald M. Barcellos,” Liahona, Mei 2025.
Mzee Ronald M.Barcellos
Sabini Mkuu mwenye Mamlaka
Akiwa na umri wa miaka 12, Mzee Ronald M. Barcellos alisoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza. Alipomaliza kusoma, alimwendea mwalimu wa seminari katika kata yake na kuuliza kama angeweza kuanza kuhudhuria madarasa ya seminari.
“Nilihudhuria seminari kuanzia umri wa miaka 12 hadi 18 kwa sababu nilipenda tu kuwepo pale na kusikiliza hadithi za Biblia na Kitabu cha Mormoni,” alisema. “Daima nimehisi upendo huu kwa ajili ya injili, na daima nilihisi ilikuwa ya kweli.”
Kuhudumu misioni baadaye kuliimarisha imani yake, na aliweka msimamo daima kuipa kipaumbele injili katika maisha yake.
“Baki karibu na [Baba wa Mbinguni], heshimu maagano yako, na mipango Yake kwa ajili yako itakamilika,” alisema.
Ronald Maldonado Barcellos alizaliwa huko São Paulo, Brazil, mnamo Novemba 4, 1975, kwa Sérgio Barcellos Silveira na Marcia Maldonado Barcellos Silveira. Alimuoa Karin Spat Albino Barcellos Silveira katika Hekalu la São Paulo Brazil mnamo Desemba 4, 1999. Wao ni wazazi wa watoto watatu.
Mzee Barcellos alisoma usimamizi wa biashara katika Chuo Kikuu cha São Marcos huko São Paulo. Kazi yake ya kitaaluma ni pamoja na kufanya kazi kwa makampuni kadhaa katika mauzo na majukumu ya masoko na kama mjasiriamali. Alishirikiana na wengine kuazisha biashara kadhaa, ikiwa ni pamoja na GreenMile, LLC, ambapo alikuwa afisa mtendaji mkuu kwa miaka kadhaa.
Mzee Barcellos hivi karibuni alihitimisha huduma yake kama rais wa misioni katika Misioni ya Lisbon Porugal. Pia amehudumu kama mshauri katika urais wa kigingi, mshiriki wa baraza kuu, rais wa Wavulana katika kigingi, askofu, mshauri katika uaskofu, kiongozi wa kikundi cha makuhani wakuu, rais wa akidi ya wazee, na mwalimu wa seminari.