Wewe Ndiwe Kristo
(Mathayo 16:16)
Tunataka watoto wetu waamini katika Yesu Kristo, wawe sehemu ya Yesu Kristo na Kanisa Lake kupitia agano, na wajitahidi kuwa kama Yesu Kristo.
Wakati mwana wetu Eli alipokuwa darasa la nne, darasa lake liliunda serikali mwigo ambapo yeye alichaguliwa na wenzake kuhudumu kama hakimu wa darasa. Siku moja hakimu kutoka Mahakama ya Wilaya ya Pili ya Utah alitembelea, akamvisha Eli joho lake rasmi na kisha akamuapisha kiapo cha ofisi ya darasa lao. Hii ilichochea katika nafsi changa ya Eli, msukumo wa kujifunza sheria na Mtoa Sheria Mwenyewe, Yesu Kristo.
Baada ya miaka ya juhudi nyingi, Eli alipokea mwaliko wa usaili kwenye mojawapo ya machaguo yake ya juu kwa ajili ya shule ya sheria. Alitamka, “Mama, niliulizwa maswali 10. Swali la mwisho lilikuwa, “Unapata kutoka wapi dira yako ya maadili? Nilisema kwamba kote katika historia binadamu wamepata mfumo wa maadili kwa kupangilia maisha yao kutoka kwenye kielelezo asili. Kielelezo asili cha maadili ninachojitahidi kupangilia maisha yangu ni kile kielelezo cha Yesu Kristo. Nilisema kama binadamu wote wangefuata mafundisho ya Yesu Kristo katika Mahubiri ya Mlimani, dunia ingekuwa mahali bora, penye amani zaidi.” Kisha usaili ukaisha, na akawaza mwenyewe, “Hizi ndizo ndoto za utotoni mwangu. Hakuna mtu katika elimu dunia anataka kusikia kuhusu Yesu Kristo.
Wiki mbili baadaye, Eli alikubaliwa na kupata ufadhili wa masomo. Kabla ya kukubali, tulitembelea chuo hiki. Shule ya sheria ilikuwa inaonekana kama kasri na ilikuwa imejengwa juu ya kilima mkabala na ziwa maridadi. Cha ajabu, tulipokuwa tunatembea kupita kwenye maktaba nzuri na ushoroba wa kuvutia, tuliona maandishi kwenye mabango na mawe yaliyochongwa sifa kutoka kwenye Mahubiri ya Mlimani.
Mahubiri ya Mlimani ni mhadhara bora wenye uwezo wa kufanya maamuzi ulio wahi kutolewa, katika mafundisho yake yote. Hakuna mahubiri mengine yanayoweza kutusaidia kuelewa vyema tabia ya Yesu Kristo, sifa Zake za kiungu, na dhumuni letu kuu la kuwa kama Yeye.
Uanafunzi wa maisha yote kwa Yesu Kristo huanza katika nyumba zetu—na katika Darasa la watoto mapema katika umri wa miezi 18. Tunataka watoto wetu waamini katika Yesu Kristo, wawe sehemu ya Yesu Kristo na Kanisa Lake kupitia agano, na wajitahidi kuwa kama Yesu Kristo.
Amini katika Yesu Kristo
Kwanza, amini katika Yesu Kristo.
Baada ya mahubiri ya mkate wa uzima, “wengi wa wafuasi wa [Bwana]” waliona ni vigumu kukubali mafundisho Yake, na “wakarudi nyuma, na hawakutembea tena pamoja naye.” Kisha Yesu akawageukia wale Thenashara na kuwauliza swali la kugusa moyo: “Je, Ninyi nanyi mwataka kuondoka?”
Petro akajibu:
“Bwana, twende kwa nani? wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
“… Nasi tumesadiki, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
Kama Petro alivyoonyesha, kuamini ni “kuwa na imani katika mtu fulani au kukubali kitu fulani kuwa ni cha kweli.” Ili imani yako iweze kukuongoza kwenye wokovu, ni lazima kiini chake kiwe katika Bwana Yesu Kristo. “Sisi … tunaonesha imani katika [Yesu] Kristo pale tunapokuwa na uhakika kwamba Yeye yupo, [ufahamu] wa sifa Zake za [kweli] [na asili], na maarifa kwamba tunajitahidi kuishi kulingana na mapenzi Yake.
Nabii wetu mpendwa, Rais Russell M. Nelson, alitangaza, “Imani katika Yesu Kristo ni msingi wa imani yote na ni mkondo wa nguvu za kiungu.”
Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watoto kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo na kupata nguvu Zake za kiungu? Hatuhitaji kuangalia mbali zaidi ya Mwokozi wetu Mwenyewe.
“[Bwana] alizungumza kwa watu, akisema:
“Tazama, mimi ni Yesu Kristo. …
“Inukeni na mje kwangu. …
“… Umati ulienda mbele, na kusukuma mikono yao ubavuni mwake, na wakaona alama za misumari katika mikono yake na katika miguu yake; na hivi walifanya wakienda mbele mmoja mmoja … na waliona na macho yao na kupapasa kwa mikono yao, na walijua ukweli na walishuhudia, wenyewe kwamba ni yeye, ambaye manabii waliandika kwamba atakuja.”
Ninawaalika kutafakari jinsi haya yanavyoweza kuonekana katika maisha ya watoto wadogo. Je, wanasikia shuhuda juu ya Yesu Kristo na injili Yake? Je, wanaona picha za staha, za kuabudu za huduma Yake na uungu Wake? Je, wanahisi na kumtambua Roho Mtakatifu akishuhudia juu ya uhalisia Wake na uungu Wake? Je, wanajua kuhusu ujumbe Wake na misheni Yake?
Kuwa wa Yesu Kristo na Kanisa Lake
Pili, Kuwa wa Yesu Kristo na Kanisa Lake.
Watu wa Mfalme Benyamini walipata badiliko kuu la moyo na kwa agano waliweka wakfu maisha yao ili kufanya mapenzi ya Mungu. Kwa sababu ya agano walilofanya na Mungu na Yesu Kristo, “waliitwa watoto wa Kristo, wanawe, na mabinti zake.” Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tuna jukumu la kimaagano la kujenga ufalme Wake na kujiandaa kwa ajili ya kurudi Kwake.
Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watoto kufanya na kushika maagano matakatifu? Katika kitabu cha kiada cha Njoo, Unifuate, katika kiambatisho A na B, tunapata vianzishi vya mazungumzo na masomo ambayo yatawezesha familia na kuwasaidia walimu na viongozi katika usimamizi wao mtakatifu wa kuwaandaa watoto kwa ajili ya maisha yote kwenye njia ya agano ya Mungu.
Kuwa kama Yesu Kristo
Tatu, kuwa kama Yesu Kristo.
Katika Kitabu cha Mormoni, Mwokozi aliwaasa wanafunzi Wake wapya walioitwa kumwiga Yeye karibu kabisa inavyowezekana: “Kwa hivyo mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Amini ninawaambia, hata kama vile nilivyo.”
Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watoto waliobatizwa na kuthibitishwa kutimiza majukumu yao ya kimaagano ya kujikusanya wao wenyewe na wengine kwa Yesu Kristo? Uanafunzi wa maisha yote unatuhitaji sisi “kuwa … watendaji wa neno, na siyo wasikilizaji tu.”
Tunapotoa mialiko kwa wanafunzi wadogo wa Bwana, tafadhali chukueni kila fursa ya kuwaelekeza, kuwaongoza, kutembea pamoja nao, na kuwasaidia wao kuipata ile Njia. Shauriana na wadogo hawa wenye thamani pale wanapojiandaa kufundisha, kushuhudia, kusali, au kuhudumu ili kwamba wawe na kujiamini na uzoefu wa shangwe katika kutimiza majukumu yao. Tafuta njia zenye mwongozo za kuwasaidia wao kuja kujua hili ni Kanisa lao na wana kazi muhimu ya kufanya katika kujiandaa kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi.
Kadiri Yesu Kristo anavyokuwa fokasi ya maisha yao, kile tunachotamani, na jinsi tunavyokitamani, kinabadilika milele. Uongofu hubadilisha kila kitu! Hubadilisha asili yetu “kwamba hatuna nia ya kutenda uovu tena, bali kutenda mema daima.” Hubadilisha jinsi tunavyotumia muda wetu, rasilimali zetu, kile tunachosoma, kutazama, kusikiliza, na kushiriki. Hubadilisha hata jinsi tunavyojibu kwa heshima, kisomi, katika usaili wakati wa kutafuta kazi.
Tunahitaji kujaza Nuru ya Yesu Kristo katika kila kona ya maisha yetu. Ikiwa sisi hatushuhudii juu ya ukweli wa uungu Wake kabla ya Yeye kuzaliwa, misheni Yake ya kiungu, na Ufufuko Wake wa kufungua gereza katika nyumba zetu na katika kila mkutano wa Kanisa hili, basi ujumbe wetu wa upendo, huduma, uaminifu, unyenyekevu, shukrani, na huruma unaweza kuwa si kitu zaidi ya hotuba ya madaha ya maandalizi juu ya mawazo ya maisha. Bila Yesu Kristo hakuna nguvu ya kubadilisha, hakuna madhumuni ya kuleta mwongozo, na hakuna suluhisho la kazi ya sulubu ya maisha. Ikiwa tutakuwa bila mipango katika uanafunzi wa Yesu Kristo, itakuwa janga kwa watoto wetu.
Tunapowaambia watoto wetu tunawapenda, je, tunawaambia pia kwamba Baba aliye Mbinguni na Mwokozi Yesu Kristo wanawapenda? Upendo wetu unaweza kufariji na kutia msukumo, lakini upendo Wao unaweza kutakasa, kuinua, na kuponya..
Yesu huyu hapaswi kuwa Yesu wa simulizi ya kubuni, au Yesu wa maneno matupu, au Yesu asiye na mwili, au Yesu asiye na mipango, au Yesu asiyejulikana, bali aliyetukuka, mwenyezi, aliyefufuka, aliyeinuliwa, mwenye kuabudiwa, mwenye nguvu, Mwana Mzaliwa Pekee wa Mungu, ambaye ni mwenye uwezo wa kuokoa. Na kama vile mtoto mdogo katika Ufilipino alivyoshuhudia kwangu katika njia ya kuvutia sana siku moja, “Sote tunastahili kuokolewa!” Katika jina tukufu na takatifu la Yeye “ambaye Mungu alimfanya kuwa upatanisho [mkuu]” Yesu Kristo, amina