2025
Je, Ni kwa Jinsi Gani Unapata Marafiki?
Desemba 2024


“Je, Ni kwa Jinsi Gani Unapata Marafiki?” Rafiki, Januari 2025, 38–39.

Majibu kutoka Kwako

Je, Ni kwa Jinsi Gani Unapata Marafiki?

Tuliwaomba watoto kote ulimwenguni kwa ajili ya baadhi ya vidokezo juu ya kupata marafiki. Hivi ndivyo walivyosema.

Picha ya uso wa msichana

Ninapata marafiki kwa kujitambulisha na kuwaonesha wageni mahali wanapotaka kupafahamu. Ninaanza kuzungumza nao na kucheza nao. Mimi ni rafiki mzuri kwa kuwasaidia marafiki zangu kwenye mapambano yao na kuwasaidia wengine wajisikie wamejumuishwa zaidi.

Presley F., umri miaka 10, British Columbia, Kanada

Picha ya uso wa mvulana

Ningesema “mambo” na kuwaalika kucheza nami na kufurahia.

Jett J., umri miaka 8, Queensland, Australia

Picha ya uso wa msichana

Kwanza sema “jambo,” na kisha uwe mkarimu.

Rachel C., umri miaka 9, South Cotabato, Ufilipino

Picha ya uso wa msichana

Ninatoa pongezi za dhati.

Haleigh H., umri miaka 10, Idaho, Marekani

Picha ya uso wa msichana

Nilileta bisi kwa rafiki yangu. Baba wa Mbinguni anatutaka tuwatumikie wengine ili tuwasaidie wahisi upendo wa Mwokozi.

Allison K., umri miaka 9, Utah, USA

Picha ya uso wa mtoto

Ninapenda kuona jinsi marafiki zangu wanavyotenda wakiwa karibu na wengine. Kitu muhimu katika kuwa rafiki yangu ni kuishi kwa viwango vizuri.

Lesley A., umri miaka 12, Mkoa wa Kati, Ghana