2025
Hujambo kutoka Estonia
Desemba 2024


“Hujambo kutoka Estonia!” Rafiki, Januari 2025, 8–9.

Hujambo kutoka Estonia!

Estonia iko Ulaya ya Kaskazini na inapakana na Bahari ya Baltic. Takribani watu milioni moja wanaishi huko.

Mwangaza wa Jua Usiku wa Manane

Wakati wa majira ya joto huko Estonia, kuna wiki chache za mwangaza wa jua usiku wa manane. Jua hutua kwa kuchelewa kuliko kawaida, likiacha mwanga mweupe angani wakati wa usiku.

Nyumba ya Msituni

Nusu ya Estonia imefunikwa na msitu! Wanyama wengi huishi msituni, ikiwa ni pamoja na pakamwitu, buku, mbwa mwitu, fisi maji, na nguruwe mwitu.

Mji Mkuu

Tallinn ni mji mkuu wa Estonia. Ni mmoja kati ya miji mikongwe katika Ulaya ya Kaskazini.

Tamasha la Wimbo na Dansi

Tamasha hili ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Estonia. Linafanyika kila baada ya miaka mitano na limekuwa na hadi watu 100,000 wanaohudhuria.

Nchi ya Kisiwa

Estonia ina zaidi ya visiwa 2,000. Vingi kati ya visiwa hivi ni vidogo mno, kwa hiyo watu wengi wanaishi bara na kwenye visiwa vikubwa.

PDF ya hadithi

Kielelezo na Greg Paprocki