2025
Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa
Desemba 2024


“Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa,” Rafiki, Januari 2025, 34–35.

Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa

Maneno kutoka Kwako

Ninajua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli na Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu. Ninaposali, ninajisikia vizuri ndani.

Dirk B., umri miaka 8, Nevada, Marekani

Chumba changu ninachokipenda katika hekalu ni chumba cha kuunganishwa. Ninajua kwamba siku moja nitafunga ndoa na kuunganishwa hekaluni kwa milele yote. Ninapenda kuliona hekalu!

Isabel R., umri miaka 10, Ceará, Brazili

Mchemraba wa Urafiki

  1. Kata mpangilio.

  2. Kunja mpangilio kwenye mistari na ugundishe vichupo mahali pa kutengeneza mchemraba.

  3. Zungusha mchemraba kwa ajili ya mawazo ya mambo ya kufanya pamoja na rafiki. (Kumbuka: Wanafamilia wanaweza pia kuwa marafiki!)

  • Tengenezeni kiburudisho. (Jaribu shayiri za usiku kucha kwenye ukurasa wa 12.)

  • Mtumikie mtu fulani. Kama unaweza, fanya hivyo kwa siri.

  • Choreni picha ya mmoja na mwingine. Msizioneshe mpaka mtakapomaliza!

  • Tengenezeni mchezo wa kucheza nje.

  • Orodhesheni vitu vitano mnavyopenda kuhusu mmoja na mwingiine.

  • Andika mawazo yako mwenyewe!

Mzingile wa Msitu

Tafuta njia yako kupitia kwenye msitu hadi nyumbani kwa akina Smith.

Mara tatu Mfululizo

Cheza na rafiki! Fanyeni zamu kuandika X au O katika nafasi mpaka mtu atakapopata tatu mfululizo.

PDF ya Shughuli

Vielelezo na Brooke Smart