“Kadi za Mahekalu,” Rafiki, Januari 2025, 12.
Kadi za Mahekalu
Hekalu la Kirtland
-
Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa baada ya Kanisa la Yesu Kristo kurejeshwa.
-
Siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka 1836, Yesu Kristo alimtembelea Joseph Smith katika Hekalu la Kirtland.
-
Wakati hekalu lilipokuwa likiwekwa wakfu, malaika walitokea!
Hekalu la Helsinki Finland
-
Wakati hekalu hili lilipofunguliwa, liliwahudumia waumini kutoka maeneo 12 yenye ukanda wa saa tofauti!
-
Kiestonia, Kifini, Kilatvia, Kilithuania, na Kirusi vyote vinazungumzwa katika hekalu hili.
-
Mnara mkubwa hekaluni umesimama futi 147 (mita 45) na umetengenezwa kwa shaba.
Hekalu la Hong Kong China
-
Rais Hinckley aliamka usiku mmoja na akachora mchoro ambao idara ya hekalu liliutumia kujenga hekalu hili.
-
Mnamo 1996, liliwekwa wakfu kuwa “mahali patakatifu pa amani” katika mji wenye shughuli nyingi.
-
Hekalu hili lina urefu wa gorofa tano.
Vielelezo na Rachel Erickson