“Siku ya Mvua Kambini,” Rafiki, Januari 2025, 16–17.
Siku ya Mvua Kambini
Kwa nini Baba wa Mbinguni hakujibu sala zake?
Hadithi ya kweli kutoka Marekani.
“Mchezo wangu ni kesho, sivyo?” Lucy aliuliza wakati mama akimfunika kitandani.
Mama alikubali kwa kichwa. “Ndiyo! Kesho jioni saa 12:00.”
Lucy hakuweza kusubiri kabisa. Alikuwa akitazamia mchezo wa kwanza wa timu yake ya softball kwa wiki kadhaa. Na mwaka huu jezi zao zilikuwa pinki! Alikuwa amefurahi sana hata ilikuwa vigumu kulala.
Lakini asubuhi iliyofuata, Lucy alitazama nje ya dirisha na kununa. Mawingu ya kijivu yenye kutia hamaki yakiwa yamening’inia angani, na vidimbwi vilikuwa kila mahali. Mvua ilikuwa imenyesha usiku kucha.
Alipiga magoti kusema sala yake ya asubuhi. “Mpendwa Baba wa Mbinguni, tafadhali saidia hali ya hewa iwe nzuri kwa ajili ya mchezo wangu wa softball jioni ya leo.”
Siku nzima shuleni, Lucy alifikiria kuhusu mchezo ule. Alivuta taswira akiwa amevaa jezi yake mpya ya pinki, akifikia kupata ushindi. Lakini nje, mvua ilikuwa bado ikinyesha na kulikuwa kumelowa.
Lucy alisema sala ya haraka akilini mwake. Baba wa Mbinguni, tafadhali lisaidie jua litokee hivi punde ili tuweze kucheza jioni ya leo.
Wakati kengele ya shule ilipogonga, Lucy alichukua begi lake la mgongoni na kukimbia nje. Aliweza kuona jua likianza kupenyeza kutoka nyuma ya mawingu!
Lakini mama alipokuja kumchukua, alikuwa na habari mbaya. “Mchezo wa jioni ya leo umefutwa,” alisema. “Samahani.”
Lucy alitazama angani. “Jua linachomoza, hata hivyo. Pengine mvua itaacha kunyesha.”
“Ninajua,” Mama alisema. “Lakini uwanja wa softball ulikuwa umefurika kutokana na maji yote. Hivyo hata kama itaacha kunyesha, pamelowa sana na tope ni jingi sana. Watapanga upya ratiba ili mchezo uwe wakati mwingine.”
Machozi yalilengalenga katika macho ya Lucy. Alikuwa amevunjika moyo sana. Kwa kweli, hakika alitaka kucheza jioni ya leo. Kwa nini Baba wa Mbinguni hakujibu sala zake?
Nyumbani, Lucy alihisi kuwa wa kijivu na mwenye manung’uniko kama mawingu ya mvua yalivyokuwa. Hakuhisi kusoma kitabu chake anachokipenda. Na ingawa Mama alitengeneza tambi zake alizozipenda kwa ajili ya chakula cha jioni, hazikuwa na ladha nzuri.
Baada ya chakula cha jioni, dada mdogo wa Lucy, Ellie, alitambaa kwenye paja lake. “Unataka Kucheza nami?” aliuliza.
Lucy alivuta pumzi. “Hakika,” alisema. Kisha akapata wazo. “Tunahitaji kufanya kitu cha kufurahisha.”
Alichukua ufagio na kufunga skafu upande mmoja ili kutengeneza bendera. Kisha akawakusanya dada zake wote. Aliinua bendera na kusema, “Karibu kwenye Siku ya Mvua Kambini! Ni mahali ambapo unakwenda kupata burudani wakati amnapo huwezi kucheza nje.”
Dada zake walishangilia.
“Kwanza,” Lucy alisema, “tutaimba wimbo wetu wa kambi.”
Wasichana walichekacheka walipokuwa wakibuni wimbo wa kijinga na maneno ya kwenda na wimbo. Kisha walitembea kuzunguka chumba na bendera yao, wakiimba kwa sauti kubwa kadiri wawezavyo.
“Sasa tunahitaji kupiga hema letu!” Lucy aliwasaidia dada zake kukusanya blanketi na mito ili kutengeneza ngome. Iliporomoka mara kadhaa. Lakini walipoirekebisha, wote walijibana ndani ya ngome ili kucheza michezo.
Punde ulifika muda wa kulala. “Natumaini mvua itanyesha tena kesho,” alisema Liza dada yake Lucy. “Nataka kucheza Siku ya Mvua Kambini tena!”
“Asante kwa kucheza na dada zako,” Mama alisema alipokuwa akimkumbatia Lucy kwa ajili ya usiku mwema. “Ulifanya mwanga wako mwenyewe wa jua kutoka kwenye hali ya mawingu. “Najivunia juu yako.”
Lucy alihisi furaha alipopanda kitandani. Sala zake hazikujibiwa jinsi alivyotaka. Lakini Baba wa Mbinguni alikuwa bado amemsaidia kupata kitu cha kufurahisha kufanya pamoja na familia yake—na hiyo ilikuwa burudani tu kama vile kuvaa pinki kwenye mchezo wake wa kwanza wa softball.
Vielelezo na Apryl Stott