“Shayiri ya Usiku Kucha,” Rafiki, Januari 2025, 32.
Hebu Tupate Kupika
Shayiri ya Usiku Kucha
-
1/2 kikombe (gm 50) Shayiri Iliyovingirishwa
-
1/2 kikombe (ml 120) maziwa
-
1/4 kikombe (ml 60) mtindi usio na viongeza ladha au wenye viongeza ladha
-
Asali au sukari nyingine
-
Vitu vya kuweka juu (karanga, matunda, vibanzi vya chokoleti, mdalasini, nk)
-
Mimina shayiri iliyovingirishwa ndani ya kopo au chombo kingine kikiwa na kifuniko. Ongeza mtindi. Mimina maziwa juu na uchanganye vizuri.
-
Funga chombo na uweke kwenye jokofu usiku mzima (au angalau masaa mawili).
-
Ongeza asali, kisha koroga shayiri na kuongeza vitu vyovyote vya kuweka juu unavyovipendelea!
Vielelezo na Alyssa Tallent