2025
Urejesho ni kwa ajili Yako
Desemba 2024


“Urejesho Ni kwa ajili Yako,” Rafiki, Januari 2025, 2–3.

Kutoka Urais wa Kwanza

Urejesho ni kwa ajili Yako

Imetoholewa kutoka, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 88–92.

Kielelezo cha familia pamoja na watoto wadogo mbele ya hekalu

Inamaanisha nini kwako kwamba injili ya Yesu Kristo imerejeshwa duniani?

Inamaanisha kwamba familia yako inaweza kuunganishwa pamoja milele! Inamaanisha kwamba wakati unapobatizwa na kuthibitishwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo, Roho Mtakatifu anaweza kuwa pamoja nawe daima. Inamaanisha kwamba nguvu za ukuhani zinaweza kukubariki kadiri unavyofanya maagano na Yeye na kuyatunza.

Nabii wa Mungu Joseph Smith ni nabii wako. Alikua nabii wa kwanza wa Kanisa lililorejeshwa. Ufunuo bado unatiririka kutoka kwa Bwana katika mchakato huu unaoendelea wa Urejesho.

Mungu yu hai! Yesu ndiye Kristo! Kanisa Lake limerejeshwa! Yeye na Baba yetu wa Mbinguni, wanatulinda.

Rejesha Picha

Nenda kwenye ukurasa wa 6 na usome kile ambacho urejesho unamaanisha. Kisha jaribu kurejesha picha hii kwa kuchora katika sehemu zinazokosekana!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Alyssa Petersen