2025
Maneno Yangu ya Injili
Desemba 2024


“Maneno Yangu ya Injili,” Rafiki, Januari 2025, 6.

Maneno Yangu ya Injili

Tafuta maneno haya na virai katika toleo hili la Rafiki!

Ono la Kwanza

Sanaa ya Karatasi ya Kijisitu Kitakatifu

Ono la Kwanza lilikuwa wakati Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walipomtembelea Joseph Smith baada ya kusali. Alitaka kujua ni kanisa gani la kujiunga nalo. Walimwambia Joseph kwamba yeye angesaidia kuanzisha Kanisa la kweli la Yesu Kristo duniani.

Kijisitu Kitakatifu

Kijisitu Kitakatifu ndipo Joseph Smith alipopata Ono la Kwanza. Ilikuwa msituni karibu na nyumba ya Joseph huko Palmyra, New York, Marekani.

Urejesho

Sanaa ya karatasi ya jengo la kanisa

Kurejesha kitu inamaanisha kukirudisha kwenye hali kama kilivyokuwa awali. Urejesho ni kile tunachokiita Yesu Kristo kuleta injili Yake ya kweli duniani. Urejesho ulianza wakati Joseph Smith alipopata Ono la Kwanza. Rais Russell M. Nelson bado anapokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa kama nabii wetu. Hii inamaanisha Urejesho unaendelea leo!

Ufunuo

Ufunuo ni jinsi Baba wa Mbinguni anavyozungumza nasi. Tunapokea ufunuo kupitia kwa Roho Mtakatifu. Anaweza kuleta hisia mioyoni mwetu na mawazo akilini mwetu.

PDF ya hadithi

Vielelezo na Maddie Baker