2025
Urejesho Unaanza
Desemba 2024


“Urejesho Unaanza,” Rafiki, Januari 2025, 24–25.

Urejesho Unaanza

Jifunze jinsi Joseph Smith alivyoongozwa kurejesha Kanisa la Yesu Kristo.

Kielelezo cha Palmyra, New York
  1. Palmyra, New York (1820): Joseph Smith na familia yake waliishi hapa. Wanafamilia wa Joseph wote walikwenda kwenye makanisa tofauti, na Joseph hakujua ni kanisa gani la kujiunga nalo. Alisoma katika Biblia, “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu” (Yakobo 1:5).

    Kielelezo cha Ono la Kwanza
  2. Kijisitu Kitakatifu (majira ya kuchipua ya mwaka 1820): Joseph Smith alisali na kumuuliza Mungu ni kanisa gani la kujiunga nao. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea yeye. Walimwambia hapaswi kujiunga na kanisa lolote. Walimwita Joseph kusaidia kurejesha injili timilifu ya Yesu Kristo duniani.

    Kielelezo cha nyumba ya Joseph Smith
  3. Chumba cha Joseph (1823): Malaika Moroni alimtembelea Joseph Smith. Alimwambia Joseph kuhusu mabamba ya dhahabu ambayo yalikuwa na injili timilifu ya Yesu Kristo. Moroni alipokuwa akizungumza, Joseph aliona ono la mahali ambapo mabamba yalikuwa yamezikwa.

    Kielelezo cha malaika Moroni akimtokea Joseph Smith juu ya Mlima Kumora
  4. Mlima Kumora (1827): Malaika Moroni alimpa Joseph Smith mabamba ya dhahabu katika Mlima Kumora. Joseph pia alipokea vyombo maalumu ambavyo vilikuwa vimezikwa pamoja na mabamba. Mungu alikuwa amevitayarisha ili kumsaidia yeye kutafsiri mabamba yale. Mabamba yaliyotafsiriwa yalikuja kuwa Kitabu cha Mormoni ili kwamba watoto wote wa Mungu waweze kusoma maneno Yake.

PDF ya hadithi

Kielelezo na Adam Koford