2025
Marafiki kote Ulimwenguni
Desemba 2024


“Marafiki ulimwenguni kote,” Rafiki, Januari 2025, 14–15.

Marafiki kote Ulimwenguni

Msichana akiwa ameshikilia mchoro wake wa hekalu

Eva B., umri miaka 6, Antwerp, Ubelgiji

Mchoro wa hekalu wa mtoto

Eduardo B., miaka 10, Pichincha, Ecuador

Mchoro wa mtoto wa Joseph Smith akipata mabamba ya dhahabu

“Joseph Smith Anapata Mabamba ya Dhahabu,” Abigail H., umri miaka 10, California, Marekani

Hekalu lililotengenezwa kwa matofali

Elizabeth J., umri miaka 8, Carolina ya Kaskazini, Marekani

Mchoro wa mtoto wa kanisa

“Kanisa Langu,” Russell J., umri miaka 9, Arkansas, Marekani

Mchoro wa mtoto wa safina ya Nuhu

Bonnie M., miaka 5, Utah, Marekani

Picha ya uso wa msichana

Lengo langu ni kushiriki talanta zangu. Ninaimba wakati kaka yangu akipiga kinanda. Ninataka kuwasaidia wengine wahisi upendo wa Mwokozi kupitia muziki.

Elena A., umri miaka 9, Puerto Rico

Picha ya uso wa mvulana

Ninafurahia kuhudhuria kanisani Jumapili na kujifunza kuhusu injili. Kuhudhuria kanisani huimarisha msingi wangu wa kiroho na hunisaidia nifanye maamuzi magumu.

Daniel C., miaka 8, Hawaii, Marekani

Picha ya uso wa mvulana

Nilihisi Baba wa Mbinguni na Yesu walikuwa karibu nami wakati wa ubatizo wangu. Ubatizo wangu ulikuwa maalumu kwa sababu nilishiriki siku ile pamoja na binamu zangu wawili ambao tuna umri sawa.

Ezra C., miaka 9, Ufalme wa Dubai, UAE

Picha ya uso wa msichana

Niliongoza muziki kwa ajili ya programu yetu ya Watoto kanisani! Ninapenda kuimba nyimbo za dini. Ilinipa msukumo kuanza kujifunza kupiga kinanda kutoka kwa mmisionari mwandamizi. Ninaweza kupiga baadhi ya nyimbo kutoka kwenye kitabu cha nyimbo za dini.

Gabriella G., umri miaka 10, Harare, Zimbabwe

Picha ya uso wa mvulana

Nina shauku ya kuwa mmisionari kama Yesu na kushiriki injili.

Luciano C, umri miaka 9, Macau, China

Picha ya uso wa msichana

Ninamtumikia Baba wa Mbinguni kwa kufanya vitendo mbalimbali vya ukarimu kwa watu.

Ellie M., umri miaka 11, Maryland, Marekani