2025
Margo na Paolo
Desemba 2024


“Margo na Paolo,” Rafiki, Januari 2025, 33.

Margo na Paolo

Bangili za Urafiki

Mama, Margo, na Paolo sokoni

Ninamkumbuka Laura. Ninachukia wakati marafiki wanapohama.

Mimi pia. Hii inaleta hisia mbaya zaidi kuliko nyakati zote ambapo sisi tulipaswa kuhama.

Mama, Margo, na Paolo wakinywa na kula asusa

Bado unaweza kumpigia simu! Au kumwandikia barua.

Ninadhani hivyo.

Margo na Paolo wakiwa wameshikilia vinywaji vyao na wakionekana kuwa na huzuni

Inasikitisha wakati marafiki wanapokwenda. Lakini tunaweza kuwa na shukrani kwa jinsi urafiki wao ulivyotubariki.

Margo na Paolo wakiangalia bangili zao

Unakumbuka wakati Laura alipotupatia bangili hizi za urafiki kwa ajili ya siku yetu ya kuzaliwa?

Ndiyo! Na alituandikia jumbe zile nzuri pia.

Mama na Margo wakizungumza wao kwa wao

Anaonekana kama rafiki mzuri.

Ndiyo! Yeye daima ni mkarimu, kama Yesu. Ninataka kuwa rafiki mzuri pia.

Mama, Margo, na Paolo wakiondoka sokoni

Eeh, labda tunaweza kutuma bangili za urafiki kwa Laura katika barua.

Acha tuwape pia Lucas na Julia!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Katie McDee